NMHabari za week end hii wadau? Hope mko poa. Leo naweka post jukwaa hili nikiomba ushauri juu ya camera bora ya kupigia picha (kikazi zaidi)
Nataka kuingia kwenye biashara hii ya picha kujiongezea kipato japo kidogo.
Sasa katika pita pita zangu (google) nikakutana na kuvutiwa na camera mbili.
1. Sony A3000
2. Nikon D90
Kwa kuangalia specs Sony anaonekana kuwa juu (20 megapixels na hd ya 1080 na vitu vingine viingi vya kuvutia pita hapa Sony A3000 First Impressions Review: Digital Photography Review.)
Tofauti na Nikon D90 ambayo ina megapixels 12.9 haina HD. Unawezapita hapa kwa more details Nikon D90 Review: Digital Photography Review
Nikajaribu kumuuliza mpiga picha mmoja kwenye harusi akasema kuwa Nikon ni bora kuliko Sony on basis kuwa Sony inatoa soft pictures ila sio quality.
Naombeni ufafanuzi juu ya ubora wa hizi Camera na kama kweli hii Sony yaweza kufaa kwa hii shughuli na hata bei zake hapa bongo (zote mbili)
Natanguliza shukurani.