Msaada kuhusu tatizo la meno kuuma

Msaada kuhusu tatizo la meno kuuma

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
964
Reaction score
2,206
Kwa muda mrefu kidogo nimekuwa nikisumbuliwa na meno hasa hasa ninapokula nyama choma. Meno yanauma (magego) kama yale yanayotikisika kama yanataka kutolewa kwa lazima na hali hii hudumu kwa siku mbili hadi tatu na mara nyingine hadi siku ya nne

Maumivi yanaenda yakipungua na nayahisi pale ninapojaribu kutafuna kitu tena hata kama ni kiraini

Tafadhali naomba msaada wenu
 
Hii ya meno imekuwa kama janga la kitaifa
 
Tatizo ni fizi, badili dawa ya meno unayotumia, sukutua na maji ya vuguvugu yenye chumvi mara kwa mara.
 
Vipi ulipata tiba???

Nina kama siku mbilitatu nikinywa vitu vyamoto naumia chini ya gego fulani.


Cc Smart911
 
Mimi nina tatizo hili la meno kuuma kila baada ya miezi kadhaa...Ila huwa sitafuti sababu maana nakula vitu vya sukari saana.... nisiingie dukani tu....
Nikishika packet ya smarties kama hakuna aliyepo karibu yangu basi 200g zinaenda,...najaribu kuacha.
 
Tafuta dawa inaitwa Colgate Sensitive Pro Relief. Tumia hiyo dawa kwa ajili ya kusafisha meno asubuhi na jioni. Tatizo lako litapungua kwa kiasi kikubwa
 
Tafuta dawa inaitwa Colgate Sensitive Pro Relief. Tumia hiyo dawa kwa ajili ya kusafisha meno asubuhi na jioni. Tatizo lako litapungua kwa kiasi kikubwa
Nashukuru, kwasasa nimeanza kutumia sensodyne nayo inatumika kama "teeth sensitive relief"
 
Back
Top Bottom