habar zenu wapendwa!!mimi naitwa mama L..... kuna ndoto ambayo inanitatanisha hivyo naomben msaada wenu kwa wale wanaojua tafsiri za ndoto.. NDOTO yangu ni kwamba uwa naota maiti zipo ndani kwangu au kma sio ndani basi zipo kwa nje ya nyumba zimening'inizwa knyw mti... na chazo cha ndoto naaza kuota kma nipo sokoni alafu anatokea mzaz mwenzie na mume wngu ananambia anamludisha mtoto sasa nikiludi nyumbani ndonakutana na hzo maiti...
Haina maana yoyote mbaya kwa sababu umekua ukiota mara kwa mara ndoto ya aina hiyo. Nimesema hivyo kwa sababu hiyo ni njia anayotumia Ibilisi kutuhadaa wanadamu
1.Ameangalia udhaifu wako katika jambo fulani na ndiyo analitumia ili kukusukuma katika kutenda uovu ambao utakua ni chukizo kwa Mwenyezi Mungu. Mfano, mwingine anaweza kuoteswa msichana mrembo fulani ambaye alisoma naye miaka mingi ya nyuma mara 2 au zaidi kila mwezi wako katika mazingira fulani japo hawakuwahi kuwa na uhusianao wowote zaidi ya kuwa maclassmate tu. Mtu wa aina hii atatekwa na unyonge amkapo na kuwaza sana hata wengine kuanza kuwasahau wake zao au wapenzi wao kwa muda wa masaa kadhaa. Wengine wanaingia katika website nakuanza kuwatafuta katika fesibuku,twita hata hapa JF wanakujaga.
Sasa wewe Ibilisi anataka akusukumie katika mambo ya KISHIRIKINA ambayo ni chukizo kwa Mwenyezi Mungu. Wewe wajua historia yako mwenyewe na unavyoishi hapo ulipo,tangu umekutana na Mumeo na huyo mzazi mwenza. Sisi hatukujui,kwa hiyo jipime mwenyewe MATENDO YAKO alafu simama kidete kupambana na hili.
Sasa ni wakati wako wa kusimama kiimani kama wewe ni Muislam simama katika Ibada ikewezeka soma vitabu vya dini pia,vivyo hivyo kama ni Mkristo simama katika ibada.Shirikisha hata viongozi wa dini katika maombi yote.
Usisahau kumuomba Mwenyezi Mungu kabla ya kulala hili ni muhimu sana. Kwa sababu ya Ibilisi anakushambulia katika ndoto.
Muombe Mwenyezi Mungu kwa kila Jambo ukila chakula,ukiingia chooni,ukienda kuoga,ukipanda gari,ukienda sokoni n.k kwa sababu ndoto za aina hii haziishi tu papo kwa papo hata kidogo.
Guudi laki