Msaada kuhusu mfuko wa Taifa wa Bima ya afya

Msaada kuhusu mfuko wa Taifa wa Bima ya afya

Rajabu Msechu

Member
Joined
Apr 13, 2016
Posts
35
Reaction score
18
Wasalaam memba wote wa Jf.

Matumaini yangu mu wazima wa afya.

Nahitaji kufahamishwa zilipo ofisi za NHIF wilaya ya Kinondoni.

Je, kwa mjasiriamali kama mimi naweza nikapata Huduma ya bima iyo pmj na familia yangu?

Gharama zake zikoje kwa mtu anayetaka kufungua daraja la tatu yaani Bronze?

Nawasilisha kwenu wajuvi wa mambo muweze kunifafanulia hili.
 
Nenda Mwenge ile barabara ya kuelekea cocacola
 
Sawa mkuu, nafika kbs kwny kiwanda cha coca au ipo nyuma ya Nabaki Africa au chuo cha tudarco?
 
Ukifika katika ofisi zao utapata maelezo ya kina,ndio inawezekana kupata wewe na familia yako!...Bima kwa kweli ni msaada mkubwa kwa sisi pangu pakavu...
 
Ila ya MTU binafsi inaumiza sana maana ni pesa nyingi 1.5m na ya vikundi ni 75,000 tuu hiyo ni familia nzima
 
Asante sana mkuu, sema ndg "Osaka" ameniambia kwa upande wa kinondoni zipo maeneo ya cocacola japo hajanifafanulia ipo kwa upande gan maana eneo lile lina ofisi nyingi
 
Duh! Kwaiyo kwa 1.5m inaisha muda gani? Na inakuwa ya watu wangapi?
 
Ila ya MTU binafsi inaumiza sana maana ni pesa nyingi 1.5m na ya vikundi ni 75,000 tuu hiyo ni familia nzima
Hiyo ya vikundi ndio ikoje mkuu ufafanuzi kidogo ndugu
 
Kama uko kwenye SACCOS nawashauri mjiunge kama kikundi huwa inakuwa na unafuu sana, enewei fika ofisini kwao watakupa maelezo, usingie peke yako gharama ni kubwa sana1.5m lakini mkiingia kama kikundi cha SACCOS inakuwa 78,000/= tu kwa mwaka
 
Back
Top Bottom