Msaada kuhusu mashine za max malipo wakuu

Msaada kuhusu mashine za max malipo wakuu

NALO LITAPITA

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
333
Reaction score
90
Wakuu mimi ni graduate, wakati fulani nilileta hapa uzi nikiomba ushauri juu ya kuanzisha huduma za mpesa, tigopesa na airtel money. Ki ukweli nilinufaika sana na michango yenu. Naomba mnisaidie kuhusu mashine au huduma ya max malipo, kuna mdau aliniambia ukiwa nayo hii huna haja ya kutafuta zile line za uwakala ambzo baadhi yake mfano tigo hawatoi. Je ni kweli kuwa ukiwa na hii mashine ya Max malipo unaweza kutoa huduma a mpesa, tigopesa na airtel money bila kuhitaji line za uwakala? Na pia ukiacha malipo kwa ajili ya LUKU na DSTV ni malipo gani mengine mtu aweza fanya kupitia Max Malipo? Mwisho naomba aliyewahi kufanya biashara kupitia mashine hizi au ambae yuko kariibu na mtu anayefanya biashara hii anisaidie kunifafanulia jinsi mtu unavyoweza kunufaika na kuwa agent wa Max Malipo. Nisaidien wakuu walau nipate kitu cha kujishughulisha nacho.
 
Kwanza hawa jamaa mashine zinasumbua sana mara mtandao hakuna pili hawajajiunga na mpesa, tigo pesa , airtel money wala easy pesa zaidi ya vocha.

Pia commision ni ndogo sana, kununia mashine ni lak 5 na salio la kuanzia ni laki 3 na nusu.

Nakushauri ukiwa na voda pesa sasa unaweza kuuza kuuza umeme, ukalipia DSTV, Startimes na DAWASCO na cammision ni 3% ya transaction.
 
Cku Hz ukiwa na mpesa ndo kila kitu hamna haja ya kuwa na max malipo maana huduma zote za max malipo wakala wa mpesa anaweza kutoa
 
hivyo hakuna sababu yakuawa na max malipo
 
Ni kweli ukiwa na maxmalipo huduma zote unatoa kwa wakati mmoja maana wanatumia network ya mitandao miwili tu lakn huduma zote wanatoa walisharekebishaga,, kama unamtaji chukua maxmalipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom