Habari wapendwa, kwanza polen na majukumu yenu ya kazi ktk kujenga taifa, Naomba kwenda moja kwa moja kwenye mada,kuna kampuni mama ambayo inahusika na usafirishaji , wao wanaajili wafanyakazi kwa msimu,kila mwaka mkataba unaisha na kuchukua mafao yao,tatizo lipo kwa hawa inapofika muda wa kuchukua mafao kunakua na mlolongo mwingi na kiswahili kisicho na tija,mfano, kwasasa msimu umefungwa na watu wanatakiwa kukaa kama mwezi mmoja ili kurudi tena kazin,lkn hawa jamaa kwakweli wamekua kero kubwa sana,majuzi baada ya watu kujaza fomu za mafao yao ya NSSF, Wakawaita NSSF mkoani ili kuwapa wafanyakaz wao semina,lkn hii semina walijua tu ni mbinu ya kukataa wafanyakazi kutoa mafao yao,, baada ya mjumbe wa NSSF kutoa maelezo yake,kuna mjumbe mmoja akauliza swali ambalo watu hawakulitarajia kabisa na nazan ilikua ni mbinu ya office,aliuliza ivi,,je! kama kuna mfanyakazi ana miezi mitano kazin anaruhusiwa kuchukua mafao yake???????? wakajibu ivi,hairuhusiwi mtu kuchukua mafao yake hata kama mkataba wake umeisha na bado ukawa endelevu,,naomba niweke apa sawa,, wao japo wanaajili kwa msimu lkn msimu unapofunguliwa wafanyakazi bado wanakua wale wale ndio wanaajili,ivo ndo NSSF wakaita ni mkataba endelevu,wakawajibu kama ndio wanachokifanya basi wafanyakazi tutahama chama,wakajibu sheria hairuhusu mfanyakazi kuama mfuko wajamii, point yao ni kua,unapoacha kaz inatakiwa ukae ndan ya miezi 4 bila account yako kua na transaction yoyote,wakati wao wafanyakazi wanasimama mwezi mmoja na baada ya hapo msimu unafunguliwa wanaporudi kama mwezi unaofuata wanaingiziwa mishahara,sasa naomba kujua je,kuna ukweli ktk hili au ni mbinu tu ya kuwazuia kuchukua mafao wafanyakazi wake,na je sheria ya NSSF inasemaje,pale mkataba wako unapoisha n kuchukua mafao yako unaruhusiwa kukaa muda gan ili account yako iingiziwe pesa upya ya mafao???? vp wafanyakazi wanaweza kupata msaada wa kisheria kuhusu hili,na kama wanaweza kupata namba za watu wajuu wa NSSF ili kupata msaada zaidi..sababu hawa NSSF mkoa wanaona kama hakuna msaada wowote wanaufanya zaidi ya kutumika na office,,.hili ni jipu,