Habari,
Nimejitokeza hapa ili nipate ufafanuzi kuhusu jar protected files. Kuna program ina content ambazo nahitaji kuzi copy kwa ajili ya matumizi binafsi lakini nimegundua kwamba iko protected. Yaani huwezi fanya chochote na hizo content zilizomo tofauti na kusoma tu. Kisha kuziacha mpaka nafikia hatua ya kuchukua kalamu na daftari nianze kukopi. Naona kufanya hivyo kunanichukua muda mrefu sana. Kuhusu zile basics za ku highlight wala ku-rightclick nazo hazifanyi kazi.
Angalau ingekua website ningetumia firefox ku disable javascript.
Hiyo program kupata access yake mpaka uwe na data connection.