Msaada kuhusu Curriculum Vitae

Msaada kuhusu Curriculum Vitae

April26

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2020
Posts
1,405
Reaction score
2,162
Habari za leo wakuu.

Naomba kuuliza swali kuhusu wasifu wa muombaji kazi (CV).

Mfn: una uzoefu wa miaka mitano (five years work experiences) halafu CV yako ina page almost 4 tu na hapo umejaribu kupunguza (minimize) kulingana na idadi ya majukumu uliyokuwa unafanya, halafu unaona tangazo linataka CV iwe na page 2 tu.

Swali, utazingatia nini kuhakikisha ile experiences ya miaka 4 ionekane kwa asilimia kubwa kwenye hizo page 2?

Ikumbukwe, CV inaeleweka inatakiwa iwe na vitu gani vya muhimu, kama taarifa binafsi, elimu labda O-level, A-level, Diploma, Degree, Masters etc, then labda Training course mfn, Computer literacy na nyinginezo.

Ni lazima kuonyesha uzoefu ulikopita hadi ulipo ikiwa unafanya kazi au lah! Mfn, umefanya taasisi 4 tofauti ndani ya miaka minne, kama vile part time, internship, contract etc, kuna kazi zina mikataba ya mwaka 1 mnamalizana.

Kama nilivosema majukumu kila taasisi haliwezi kuwa moja lazima uonyeshe umefanya nini lini hadi lini, hii hufanya CV kuwa ndefu.

Kama nilivyouliza, swali, utazingatia nini kuhakikisha ile experiences ya miaka 4 ionekane kwa asilimia kubwa kwenye hizo page 2 bila kuathiri chochote?

NB: Kuna baadhi ya mataifa wana mtindo almost unao fanana wa CV japo unaweza kuwa una utofauti kati ya mtu na mtu.Je Tanzania/Africa mashariki tuna format ya CV inayotambulika kama ilivyo Ulaya na Marekani?

Ahsanteni
 
Una miaka mitano kazini unaandika elimu ya sekondari ulisoma wapi ili iweje. Umefika chuo, umefanya kazi miaka minne bado kuna mtu anataka kuhakikisha kama umesoma kidato cha nne? Sidhani

Futa hizo sekondari taja diploma, degree na kuendelea na uongeze training ulizoenda na uzoefu wa kazi. Kama una degree pekee kwenye elimu andika hiyo tu
 
Una miaka mitano kazini unaandika elimu ya sekondari ulisoma wapi ili iweje. Umefika chuo, umefanya kazi miaka minne bado kuna mtu anataka kuhakikisha kama umesoma kidato cha nne? Sidhani...
Oky, hiyo format inakaaje mkuu.

Unaweza kunisaidia format ya jinsi hiyo?
 
Tengeneza kitu kama hiki
672f09fe54ce807442c7dcc75f9f45cc.jpg
 
Una miaka mitano kazini unaandika elimu ya sekondari ulisoma wapi ili iweje. Umefika chuo, umefanya kazi miaka minne bado kuna mtu anataka kuhakikisha kama umesoma kidato cha nne? Sidhani

Futa hizo sekondari taja diploma, degree na kuendelea na uongeze training ulizoenda na uzoefu wa kazi. Kama una degree pekee kwenye elimu andika hiyo tu
Hapana, kama taasisi watataka kufanya vetting hiyo ya kuondoa elimu za awali litafanya limitation
 
Mtoa mada nahisi ulivypangilia CV yako ndio shida inakuja..
hapo swala ni upangiliaji na matumizi sahihi ya fonts and fonts size + tables and data sorting je umefanya alignment ipi.. etc.
 
Mtoa mada nahisi ulivypangilia CV yako ndio shida inakuja..
hapo swala ni upangiliaji na matumizi sahihi ya fonts and fonts size + tables and data sorting je umefanya alignment ipi.. etc.
Nishapata ufumbuzi mkuu.
 
Back
Top Bottom