Haya fanya kama ifuatavyo
Wakati computer inawaka ikivuka BIOS Screen (kabla ya windows logo kutokea) haraka bonyeza F8 uwezavyo hata ka ni mara kumi hadi uone screen imekuja ina options kama "Safe mode, Safe mode with networking etc" utachagua option "Repair computer"
hii nimefanya assumption unatumia Windows Vista, 7 au 8 maana kwa wale wa XP hii trick haifanyi kazi kama ni xp itabidi ufanye tu repair kwa kutumia cd ya xp ya kawaida...
Haya tuendelee, ukishaweka repair itakua inaitwa System Recovery Options
Utachagua Local disk yako ambayo ndio ina main system kama ni "C" afu utaclick "Load drivers"
Itakufungulia options ka inayotokea ile ukiwa unasave file.. Click Computer then utaona local disk C.. right click then nenda properties..
Tafuta sehemu inakibox kitakua kimetikiwa "Compress this drive to save space" toa hiyo tiki, afu apply... italeta options nyingine chagua apply changes to folder and subfolders tiki... itachukua muda, ikimaliza we cancel kila kitu, zima washa machine. piga mzigo kama kawaida..