Nina kijana wangu kamaliza kidato cha sita mwaka huu, sasa kuna rafiki zake wanamchanganya kuhusu chuo. Kila mara anaongelea kuhusu Archbishop James University (AJUCO) kilichopo Songea, na imekuwa kero kwangu sana. Naomba anayekijua chuo hiki kwa habari ya ubora wa taaluma. Hasa kwa upande wa sayansi.
Asante mkuuhiki chuo mii nakijua na kuna best angu yupo pale anachukua md first year, alisoma cbg alipata 1 ya 7,, ni chuo kizur hakina competion sana kwa md,, kipo nnje kdg ya songea kwa kozi za md, kwa edction kpo toun pale pale,,,
Kiongozi kama umeniona vile! Jana tu ametoka kupewa mkong'oto. Yaani alitaka yeye ndio awe baba ndani ya nyumba. Lakini baada ya hasira kutulia na ndipo nikaomba ushauri japo kuwa yeye hajui kinachoendelea.Mikijana wangu aliwahi kuniletea mambo ya marafiki....
Nilichokifanya nilimpa makonde ya haja, alafu nikapiga kimya kama wiki moja hivi.... No salam. Mwisho nilimuambia akitaka tuende sawa, anapaswa tukae mezani Mimi na yeye na kisha anieleze kila anacho kihitaji na lazima anipe sababu (ushawishi).
Baada ya hapo tulielewana mimi na yeye, na nikamwambia sitaki habari za marafiki
Ipo siku atakuja kukuangusha mbele za watu,kuna dogo alikuwa anapigana na baba ake.Kiongozi kama umeniona vile! Jana tu ametoka kupewa mkong'oto. Yaani alitaka yeye ndio awe baba ndani ya nyumba. Lakini baada ya hasira kutulia na ndipo nikaomba ushauri japo kuwa yeye hajui kinachoendelea.
Ana bahati mbaya amezaliwa na mimi, maana moto wake anajua vema. Nami sipendi hata kidogo kupiga watoto. Huyu nafikiri huko boarding alikokuwa ndio kumempa ujeuri. Nami nimeona nimpashe mara ya mwisho ajue bado sijazeeka akasimulie huko chuoni anakotaka kwenda mkuu. Asijifanye baba kwenye nyumba yangu.Ipo siku atakuja kukuangusha mbele za watu,kuna dogo alikuwa anapigana na baba ake.
Asante mkuu! Hawa watoto wa miaka hii!!Mkuu,
Hiyo ni dhana na tatizo kubwa sana kwa vijana wetu. Punde tu baada ya kumaliza elimu yao ya Sekondari ya Juu, huwaza zaidi kuhusu kujiunga na Chuo. Hujidanganya na kuokoteza Uongo wa hapa na pale. Uongo huo na ushauri wanaopeana, hujijaza ujinga na uzandiki.
Yaani, kila Mara wao huwaza tu kuhusu kujiunga Chuo hata kabla ya matokeo kutoka. Sikatai wao kujishauri, La hasha!. Lakini, kujijaza ujinga ni aina mbaya ya tabia.
Cha msingi kaa naye chini, tafuta details za kutosha kuhusu Chuo husika. Muambie kwa nini anadhani Chuo hicho ni kizuri?
Muambie katika maelezo yake ajikite zaidi katika maeneo haya;
1) Mazingira ya Chuo
2) Ubora wa vifaa na walimu
3) Ushindani wa wataalamu wao baada ya kuhitimu.
Nakuhakikishia hana lolote analolijua. Wanadanganya tu kwenye magroup yako ya WhatsApp.
Unaweza kufatilia kuhusu hicho Chuo huku mitandaoni.
Asante mkuu kwa ushauri wako.Pole sana mkuu
Mara nyingi vyuo vya private vipo kibiashara zaidi na ndio maana unaona promotion. Sababu system ya udahili imebadilishwa kila chuo cha private kinatumia mbinu kuvutia wateja hususani kwenye magazeti
Kinachotakiwa mtulize huyo kijana wako mwambie asubiri matokeo ndio process zingine ziendelee
Akifaulu vizur omba Udsm, Muhammad, udom, kcmc na bugando vyote medicine na course zingine za afya
Ulicho fanya ndio sahihi huu ni wakati mgumu kwa wazazi wengi. Watoto wana group _thinking. Issue kubwa itakuwa kuoanisha ufaulu wake na uchaguzi wake. Ushindani wa kuingia AJUCO si mkubwa kama ule wa MUHAS na vijana wengi last year walikosa nafasi za kusomea MD. Kama utapata mtu anaekifahamu uzungumze nae itasaidia zaidi lakini always kuna element ya risk kwenye mambo haya.Ni kweli mkuu kama ulivyosema. Kuna baadhi ya vyuo ambavyo mimi ninavifahamu. Lakini kelele za huyu kijana zimenifanya niombe ushauri kwa wadau wengine wanaweza kuwa wanakijua hiki chuo pia ili kama kina ubora nimkubalie.