Msaada kuhusu barua ya posa

Mzee Mtambuzi kijana anataka barua ya POSA sio KUTONGOZA.

Lizyy we si una Mume? Tuwekee sempo iliyowalainisha wazee wako wakasarendaa! Vinginevyo nakumbuka ile thread flan ilikuwa inasema ' MANENO TU ANA.........MWENYEWE'

Kama gumu kalale!
 
 
Lizyy we si una Mume? Tuwekee sempo iliyowalainisha wazee wako wakasarendaa! Vinginevyo nakumbuka ile thread flan ilikuwa inasema ' MANENO TU ANA.........MWENYEWE'

Kama gumu kalale!
Hamna cha barua wala nini. Kaenda mwenyewe akawaambia ana kwa ana "binti yenu nataka kumuoa sasa nimekuja mnipe taratibu na mahitaji ya kukamilisha hilo.". . .kazi kwisha.
 
Ndugu wanajf wa jinsia ya kiume naombeni msaada wenu juu ya kuandika barua ya posa,je ni maneno gani huandikwa ndani ya barua ya posa na pia muundo wake ukoje?natumaini wanaume wenzangu wanao jua hili suala watanifahamisha.
BAADA YA KUWEKA ANUANI YAKO.

Kwenu wazazi wa (unaweka majina mawili au matatu tufanye labda Kalunde Biringanya Mananasi)
Mimi naitwa Kisiki kama navyosomeka kwenye anuani hapo juu
kwa heshima kubwa niliyonayo kwenu wazazi wa Kalunde Biringanya Mananasi na bila kushawishiwa na mtu yeyote,kwa akili yangu timamu mimi Kisiki Abunuwasi Kalumekenge nimekuandikieni barua hii yenye maombi ya kukubaliwa kumposa binti yenu Kalunde Biringanya Mananasi .Umri wangu ni miaka (taja miaka yako).
Endapo mungu akininyooshea njia mkanikubalia,basi kwa waraka huu natangaza kumposa rasmi binti yenu Kalunde Biringanya binti Mananasi kuwa mke wangu mtarajiwa.
Nimatumaini yangu mtanipokea maombi yangu mimi
Kisiki Abunuwasi Kalumekenge.
 
we andika tu! mzee mi nimemsalandia binti yako na amenielewa na sasa nataka nimchukuea mazima, usisahahu kutia hela kidogo kwenye hiyo barua ikiwa dola watakuelewa mapema zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…