Msaada: Kozi ya kusoma ukimaliza kidato cha sita kabla ya kwenda chuo

diuretic

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
355
605
Habari za jioni wakuu, nimemaliza kidato cha sita mwaka huu na sijabahatika kuchaguliwa jkt. Nimesoma Pcm nilikua nina mpango wa kuongeza elimu kabla ya kwenda chuo. Nahitaji msaada wa mawazo ya nini cha kusoma kipindi hiki nikisubiria chuo. Kama una idea ya kozi yoyote msaada wako unahitajika.
 
hizi ni short courses kwa wale wanaosubir kwenda vyuoni. mda unategemea programs unazotaka kusoma. Zinapatikana maeneo mengi tu ya mjini.
 
Nenda kasome Basic Computer kama jamaa alivyo sema, mdogo wangu alifanya vile mwakajana,unapata na cheti kabisa.Gharama zake ni nafuu sana,VETA ni chini ya laki 2.
Ni nzuri sana hiyo mdau
 
Leseni ni kitu cha muhimu sana...unaweza ukaenda omba kazi na vyeti vyako baada ya kumaliza chuo ukaambiwa kazi hakuna kwa mujibu wa qulification zako labda kama una leseni upewe udereva! Na kampuni nyingi zinaanza hivyo...
 
Mtoa post Mawazo umepewa uchaguzi ni wako,kuwa dereva wa FUSSO,CANTER,NK,ila kumbuka hao madereva huku mtaani ni wengi kuliko unavyodhani,sisi tulikushauri computer Basics,kwakuwa ajua utajiunga Chuo Kikuu,tena na HIYO PCM,nadhani utasoma kozi zinazohitaji application ya computer,vilevile mwaka wa kwanza computer ni somo la lazima kwa wanafunzi wote,sasa ukiwa una ABC za computer itakuwa nzuri,pia sitegemei mwanafunzi wa chuo kikuu utashindwa kusoma udereva unatolewa kwa wiki 2 tu hata likizo utajisomea
 
Computer hata km hujui ukifika chuo one or two weeks utaelekezwa na roommate ni km simu tu yenye os ambayo hujawah itumia ukielekezwa unaweza faster tu mm nlienda chuo cjui hata kushika mouse ila baada ya mwez nikawa mtundu kuliko hata walokua wanajua baadae nkawawa nawawekea windows nakuzicrack hao hao walonifundsha. My advice nenda driving itakusaidia sana baada ya kumaliza chuo
 
Soma driving upate leseni yako ya gari.
me najuta kusoma introduction to computer,nililipia 170,000 for time wasting! course ya kijinga.nimeenda chuo nimesoma IT miaka yote mitatu (nilikuwa facult ya masomo ya biashara japo sikumajor IT),nikaona ile course ilikuwa ni upuuzi tuu.eti kuwasha na kuzima PC,ms word kidogo sana,excel ya kulashia,internet na email ya juujuu.bora ningesoma driving aisee najuta.kama unaenda chuo IT Utakutana nayo tena utasoma deep kidogo kuliko hata hz course za mitaani.hadi leo sijachukua cheti changu cha ile course ya mwezi.nikiangalia kwenye cheti nna matokeo ya IT semester zote sita.
 
kwa soko la ajira lilivyo jiandae kupata elimu ya kutafuta pesa kwa kujiajiri,au bora usome driving.course ya IT ukiisoma saiv halaf ukaenda chuo ukaisoma hata semester moja,utagundua kuwa ulipoteza muda na hela.ukishindwa bora utafute kazi yoyote ya ufundi ujifunze mfano fundi gereji,ujenzi wa nyumba,fundi sofa/seremala,umeme,fundi redio na tv,kuchomelea,madirisha ya alminium etc.utakuwa umeingiza kitu kikubwa sana kuliko kusoma computer halaf unafundishwa vtu ambavyo ukiwa na computer tuu unavijua kiurahisi.me nishamaliza chuo najuta maana haya niliyokushauri sikuyafanya baada ya kuhutimu la saba then form four. kidato cha sita nikasoma computer mwez mmoja(iliyobaki nilikuwa nacheza).saiv nasubiri ajira toka serikalini na sina fani yoyote.naishia kufundisha tuition uchwara mana na umri huu noma kuanza kutumwa spana na fundi niliyemzid umri.
 
Back
Top Bottom