MahinaVeterani
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 710
- 257
Wakuu, heshima kwenu na Heri ya Mwaka Mpya!
Ni ukweli usiopingika kuwa wengi wetu tunakwama katika jitihada zetu za kutaka kujikwamua kupitia Ujasiriamali hususani katika shughuli za Kilimo na Ufugaji kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na Elimu ya kutosha katika shughuli hizo. Matokeo yake kufanya shughuli hizo kwa kubahatisha, ujanjaujanja, kwa kukosa Tija na hatimaye kupoteza mwelekeo na kukata tamaa.
Kwa mantiki hiyo, mimi binafsi (Mstaafu Mtarajiwa) nimekuwa na utashi wa hali ya juu, kurudi Shule/Chuo maalumu kwa ajili ya Kozi fupi/Mafunzo ya muda mfupi rasmi ya Kilimo na Ufugaji. Utashi huu umekuwa mkubwa sana hasa kwa Mwaka huu wa 2014. Ninapendelea zaidi Kozi/Mafunzo yasiyozidi miezi 3.
Ninaomba basi, kutoka kwenu Wadau Waheshiwa, kujuzwa ni Chuo kipi hapa Nchini kinatoa Kozi/Mafunzo mafupi (miezi 1 - 3), lini Kozi/Mafunzo hayo yanatolewa na ikiwezekana gharama zake.
Natanguliza shukrani zangu za dhati!
Chuo Kikuu huria wanatoa kozi fupi za ufugaji kuku kwa biashara.. ila bado hawajaliteka soko vema...Wakuu, heshima kwenu na Heri ya Mwaka Mpya!
Ni ukweli usiopingika kuwa wengi wetu tunakwama katika jitihada zetu za kutaka kujikwamua kupitia Ujasiriamali hususani katika shughuli za Kilimo na Ufugaji kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na Elimu ya kutosha katika shughuli hizo. Matokeo yake kufanya shughuli hizo kwa kubahatisha, ujanjaujanja, kwa kukosa Tija na hatimaye kupoteza mwelekeo na kukata tamaa.
Kwa mantiki hiyo, mimi binafsi (Mstaafu Mtarajiwa) nimekuwa na utashi wa hali ya juu, kurudi Shule/Chuo maalumu kwa ajili ya Kozi fupi/Mafunzo ya muda mfupi rasmi ya Kilimo na Ufugaji. Utashi huu umekuwa mkubwa sana hasa kwa Mwaka huu wa 2014. Ninapendelea zaidi Kozi/Mafunzo yasiyozidi miezi 3.
Ninaomba basi, kutoka kwenu Wadau Waheshiwa, kujuzwa ni Chuo kipi hapa Nchini kinatoa Kozi/Mafunzo mafupi (miezi 1 - 3), lini Kozi/Mafunzo hayo yanatolewa na ikiwezekana gharama zake.
Natanguliza shukrani zangu za dhati!
Siku hizi vinaitwa LITA( LIVESTOCK TRAINING AGENCY)hongera kwa wazo lako, ila ukipenda kusomea kitu kimoja maalum ni vizuri pia mfano hiyo ya poultry OUT, kuna ya uyoga TIRDO sijui kama bado wanatoa au SUA. Kusindika mazao mbalimbali hutolewa na SIDO. Kuna AMAGRO wanafundisha kilimo na kila kitu kuhusu maembe ukiwa umejiunga na kuwa mwanachama. Pia Online kuna kozi na mafunzo mengi hata JF mbona watu tunajifunza na kupata ujuzi lakini ukiwa unataka upate cheti na ukitumie basi nenda tu chuo hasa SUA au vya LITI.