Msaada kilimo cha hoho

Jamani acheni tu, nina matikiti yanaharibikia ndani. Watu wananunua kwa shida kwani wanasema soko no baya sana. Kilimo ni wendawazimu.
 
duu aisee mimi ninazo izo pilipili ila sijajua pakuzipeleka

Mkuu thread Ina page mbili tu lkn umeshindwa kusoma, usiwe mvivu wa kusoma boss utapitwa na fursa. Soma comments zote za wadau utapata contacts za watu wanao hitaji mzigo
 
Mzigo huo wadau nishalima
Mkuu naomba msaada wa elimu. Nina shamba maeneo ya kisarawe nataka kulima Pilipili mbuzi. Naomba kujua yafuatayo:-

1. Ni mwezi gani ninatakiwa kulima na kupanda?

2. Mbegu bora, mbolea na dawa.

3. Mahitaji mengine muhimu.

Natanguliza shukrani.
 
Matikiti bado yapo? Please write me back

Mkuu niliishia kuyauza kwa bei ya kutupa na mengi yaliharibika nikawapa mbuzi. Mkuu mm kwangu kilimo kimeniachia maumivu yasiyoisha. Mpaka najiuliza kweli Adam na Hawa walipelekwa bustanini? Mbona sisi wa shambani ndio tunaumia sana wakati watu wa maofisini wanaishi vizuri?
 
Mkuu kulima ni hatua ya kwanza, hatua ya pili ni soko. Tafuta soko wiki 4 kabla ya kuvuna. Mm nipo dar pale buguruni kuna soko zuri sana la matikiti maji. Ningekusaidia kufanya mipango ukauza vizuri tu. Usikate tamaa. Chukulia kama ni funzo kwa jaribu ulilopata.
 
Sawa mkuu
 
Wadau naomba ushauri kuhusu soko la cherry tomatoes (red and yellow) kwa mkoa wa dar. Nimelima morogoro natarajia kuvuna baada yya miezi miwili
 
utofauti wake ni kwenye kukomaa...zikianza kukomaa zinaanza kuwa njano mpaka kua nyekundu...zikiwa green zinakua bado hazijakomaa....hope umenisoma...
Sio kweli, hizo ni mbili tofauti hata ladha ni tofauti
 
 
Wakuu Mimi ndio nimeshalisafisha Shamba natafuta mteja ili nikianza kulima nianze nikiwa na focus kumit description demand ya mteja, eg, anataka hoho nyekundu, au njano au green, kama anapreference ya seed ambayo angependa niitumie, in short ni kucustomize hoho ili kumit wat the customer wants. Nna greenhouse 2 zenyekuweza kuchukua miche 600 kila moja.
 
Habari, ndugu mimi ni mgeni kbs ktk kilimo ila sasa nimeamua kulima hasa pilipili hoho, naombeni eleimu ya zao hilo, Ahsanteeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…