Mzee inaonekana ushaharibu mambo huko pole sana. Yah, ni possible kwa mwanamke kupata mimba siku ya 22 au 23 ya mzunguko wake. Si wanawake wote wana mzunguko sawasawa. Wapo wale ambao mzunguko wao unakwenda siku 21, wengine 28 na wengine 35 na kuna wengine ambao siku zao zinabadilika kila mwezi. So usirely kwenye siku ya 14 ambayo wengi wanaelekezwa.
Kuhusu kupasuka kwa kondom, hili ni jambo ambalo linatokea kwa nadra. Linaweza kusababishwa na ubora mdogo wa kondom au kukauka kwa majimaji kule mahali na kufanya msuguano ufanyike mahali pakavu. Hili pia husababisha mchubuko kwa mwanamme na mwanamke. Ni vema kubadilisha kondom mara uonapo imekuwa kavu. Si lazima kwamba condom moja itumike hadi mwisho. Ikitokea kondom imekauka kabla hujamaliza basi ibadilishe.
Hope maoni haya yamekusaidia.