Msaada kazi ya kujishikiza wakati huu

Msaada kazi ya kujishikiza wakati huu

Hey There

Senior Member
Joined
Nov 12, 2023
Posts
120
Reaction score
372
Habari,

Kwasasa sina kazi, nilikuwa nafanya kazi kwa wachina mwezi May kampuni ikapunguza wafanya kazi kutokana na sababu za kiuchumi.

Mwezi uliopita nime Apply sana kazi bado naendelea kufanya Applications na kwenda interviews mwisho jana kwahili hakuna tatizo na naamini nitapata kazi nyengine sio muda. Changamoto iliyopo PESA.

Wakati huu wakutafuta kazi inahitajika pesa sana kuwa na bando, kwenda interview, Copy and printing nk pia ujikimu inakuwa changamoto. Now nafanya udalali tu nipate pesa za kufanya mambo yote tatizo kupata pesa endelevu mtihani leo ume dalalia simu umepata 20,000 week inapita mazima.

Kwasasa naombeni msaada wenu, natafuta sehemu yoyote ambayo nitajishikiza hata kwa malipo ya 3000 kwasiku nisikaukiwe za kutafuta kazi.

Au kama una mzigo wowote mjini unatafuta wakumtuma kupeleka mimi nipo hapa kwa kazi.
M
 
Back
Top Bottom