Akizidiwa na shida, na asione mbele wala nyuma, ajisalimishe kwa balozi wetu Masilingi.
Watanzania hata huko Boston wapo wengi na naamini kuna jumuiya za watanzania miji mbali mbali huko marekani.
Ningemshauri angetafuta hizo jumiya awaeleze shida yake, naamini lazima atakuwepo wa kumsaidia hata kwa kumsitiri kwa muda akiwa anajipanga kama anavyoeleza yeye. Sifahamu ni msaada gani anauhitaji kwako mleta mada, lakini kama haupo marekani unadhani utamsaidia vipi?! Kuleta hapa jukwaani ni njia moja lakini pale ground sijui anamudu vipi kama hana kazi kabisa.
Yeye binafsi angejisaidia kwa kutafuta jumuiya za watanzania zilizopo hapo Boston au miji ya jirani, au hata nje ya state hiyo ikibidi. Sijui ukubwa wa tatizo lake kiuhalisia licha ya mleta mada kulieleza hapo kijuu juu lakini naweza kushauri ajitahidi kutafuta watanzania hapo mjini wanaweza kumsaidia kwa namna moja au nyingine.