Habari za mwaka mpya ndugu zangu.
JUZI Mrs alikuwa anasumbuliwa na mafua pamoja na kichwa ambavyo vimedumu Kwa mda mrefu Sasa, ikabidi nimpeleke hospitalini.
Alipoeleza dalili hizo Swali la dokta:au una ukimwi?.
Akamwambia inabidi ukacheki damu!!!
Nilipofatilia vipimo alivyofanyiwa nikakuta kapimwa:
1.urine analysis(kama sijakosea)
2.Hb level test
3.Mrdt
Na vyote hakuonekana ana tatizo
Sasa mkanganyiko wangu ni kutokana na swali alilouliza daktari ya Kwimba:au una ukimwi?
Nilidhani alipomwambia ukacheki damu nilitegemea angeenda kupimwa ukimwi Lakini akaandikiwa vipimo tajwa hapo juu.
Ndugu wanabodi Hilo Suala langu limekaaje kitaalamu?msaasa tafadhali!!!