Lady Ra
JF-Expert Member
- Mar 23, 2014
- 879
- 991
Wakuu habari zenu,
Mimi ni mkulima mjasiriamali, nalima mwenyewe na kuuza pamoja nanunua kutoka kwa wakulima wenzangu mazao mbalimbali na kuuza pia. Pia nafanya ufugaji wa Kuku na Mbuzi na hivi karibuni nitaanza kufuga na Samaki pia.
Katika shughuli hizi za Ujasiriamali nimebahatika kupata masoko mawili matatu ambayo wahusika wanataka kunilipa kwa mtindo wa 'formal' payment. Yaani nawapelekea kwanza "Quotation/Proforma Invoice", wanaikagua wakiridhika wananipa "Purchase Order" then nawatumia Mzigo with "Delivery Note" kisha "Invoice" wanafanya malipo. Sasa taratibu zote hizi zinanihitaji niwe na biashara ambayo imesajiliwa kwani hata malipo yao walipenda walipe kwa registered company/entity na sio kwa jina langu binafsi.
Ningependa kufahamishwa yafuatayo,
1) Kwa aina ya shughuli zangu nazozifanya, je natakiwa nifungue kampuni/taasis/shirika la aina gani??
2) Wapi au ofisi gani ya serikali hasa inahusika kusajili biashara ya aina hii?
3) Taratibu za kufuata ni zipi ili kuweza kufungua hii aina ya biashara?
4) Any additional help/idea on this
Natanguliza Shukurani
======
Jina la biashara ni jina ambalo mtu au vyombo vingine vya kisheria, huuzia biashara. Jina hilo si kama linakutambulisha wewe na wateja wako tu, hukuwezesha pia kutofautisha na washindani wako kuonyesha msisimko wa biashara yako. Kwa biashara nyingi, jina mara ni rasilimali ya thamani kubwa sana.
Masharti:
Taasisi za usajili wa biashara Tanzania
Usajili wa biashara Tanzania huanzia BRELA. BRELA ni wakala wa usajili na leseni Tanzania.
BRELA ni taasisi ya serikali na ndiyo iliyopewa mamlaka ya kasajili biashara zote Tanzania iwe ni kampuni, mtu binafsi ama biashara ya ubia.
Mfanyabiashara akishasajiliwa na BRELA anapaswa kuanza kufanya taratibu za kupata leseni ya biashara ambayo hutolewa na wizara ya viwanda na biashara ama mamlaka za halmashauri alipo.
Kwa kawaida kabla leseni ya biashara haijatolewa maafisa biashara watataka kujiridhisha kama mfanyabiashara ametimiza vigezo na masharti ya kufanya biashara anayoombea leseni. Mathalan muuza madawa na vyakula vya binadam anapaswa kusajiliwa na kuwa na cheti cha mamlaka ya chakula na madawa (TFDA).
Pia maafisa biashara watataka kujiridhisha kama huyo mfanyabiashara amejisajili mamlaka ya mapato (TRA) na ana cheti cha usajili wa mlipa kodi.
Mamlaka muhimu katika usajili wa biashara
BRELA: http://www.brela.go.tz
Wizara ya viwanda na biashara: http://www.mit.go.tz
Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC): www.tic.co.tz
=====
Imekuwa ni kawaida kwa watu hapa nchini kufanya biashara bila kufuata taratibu na kanuni za kisheria.
Ni kutokana na kutojali sheria na kanuni, wapo watu ambao hujikuta katika wakati mgumu ikiwa ni pamoja na kufilisiwa biashara zao.
Sababu ya kufilisiwa inaweza kuwa ni kutokana na kuingia mikataba bila kujua taratibu za sheria za kibiashara. Wapo ambao kwa sababu ya kutojua sheria na kanuni za biashara wamekuwa wakiingia kwenye migogoro na Serikali au watu binafsi kimakosa.
Ninachotaka kusema katika safu hii ni kwamba kabla ya kuanzisha biashara yoyote, penda kuifahamu biashara hiyo kisheria; kwa mfano unataka kufanya biashara ya kuuza ngozi ya ng’ombe, kuuza dawa za wanyama au binadamu, sheria zinasemaje hasa?
Ni mambo muhimu sana kuyafahamu. Wapo watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na sheria, sababu kubwa ni wao wenyewe kuanzisha biashara pasipo kuangalia hasa sheria zinasemaje.
Biashara ni nini? Ni shughuli yoyote inayohusisha uuzaji na ununuzi wa vitu au huduma yoyote, kwa lengo la kupata faida. Biashara inaweza kufanywa na mtu binafsi (sole proprietorship), kampuni au kwa kuingia kwenye ubia.
Mfanyabiashara binafsi ni nani? Ni mtu yeyote aliyeamua kuanzisha biashara yoyote akiwa mmiliki pekee ambaye atakuwa ametoa mtaji wake mwenyewe, faida na hasara zote zinakuwa kwake.
Sheria za biashara nchini; Sheria zinazosimamia uanzishaji wa biashara ni zikiwamo zile za usajili wa majina ya biashara (Business names Registration Act Cap 213) na Sheria ya Kodi ya Mapato ( The Income Tax Act). Pia sheria ya Leseni za Biashara Sura ya 208 (The Business Licence Act Cap 208).
Sheria nyingine zinategemeana na aina ya biashara yako mfano, kama ni biashara ya dawa utahitaji kibali cha Taasisi ya Chakula na Dawa (Tanzania Food and Drugs Authority;TFDA).
Nimelazimika kuyatumia haya maneno ya kiingereza kutokana na ukweli kuwa ndiyo tunayokutana nayo tunapokwenda kusajili, kwani Kiingereza kinafahamika nchini kama lugha ya kiofisi.
Utaratibu wa kufuata ili kuanzisha biashara
Ukishakuwa na mtaji pamoja na nia ya kuanzisha biashara, hatua ya kwanza ni kusajili jina la biashara kwa Wakala wa Usajili wa Biashara (BRERA; Business Regulatory and License Agency).
Pili, unatakiwa kuwa na leseni ya biashara ambayo hupatikana katika ofisi za manispaa husika chini ya Sheria ya Leseni ya Biashara Sura ya 208 kifungu cha 3 ambacho kinasema ni marufuku kufanya biashara bila kuwa na leseni halali katika eneo halali.
Tatu unatakiwa kwenda TRA na kupata namba ya mlipa kodi au kwa lugha ya Kiingereza Tax Identification Number (TIN).
Vibali vingine vitatolewa kulingana na shughuli unayotaka kuifanya, kwa mfano kuna biashara zinalazimisha uwe na vibali kutoka Shirika la Viwango la Taifa (TBS), TFDA, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Baraza la Wakala wa Usalama na Afya mahala pakazi (OSHA) na vinginevyo.
Faida za kuwa mfanyabiashara binafsi
Mfanyabiashara binafsi ana faida nyingi ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba hata uanzishaji wake ni rahisi, faida zinakuja moja kwa moja kwa mfanyabishara, kuingiza mshirika mwingine ni rahisi, uanzishaji wake hauna gharama sana, ni rahisi kuibadili na kufuata aina nyingine ya kufanya biashara.

Mimi ni entrepreneur nakopesha mitaan kwa riba nataka kusajiri hii biashara yangu ili niweze kulipa kodi naomba kujulishwa nianzie wapi?
na inawezekana kupata kibari cha kukopesha pesa kwa Riba?
Habari wanaJF,
Kama mnavoona tz ya viwanda nasi tunang'ang'ana
Tumejiorganise jamaa kama watatu hivi tukapata kama 50m hv tunataka kufungua kiwanda kiuchu tumesajili brela na tumekuwa certified ila isue kwa TRA hatujui procedure hata moja.
Mana nasikia mpaka kwa wizara ya viwanda ila hatui
Kwa niaba ya wenzangu nataka kuuliza kama kun yoyote mwenye info zaidi please share nasi isije kukuta mtaji wote ukaliwa kodi
JF, great thinkers
======
Jina la biashara ni jina ambalo mtu au vyombo vingine vya kisheria, huuzia biashara. Jina hilo si kama linakutambulisha wewe na wateja wako tu, hukuwezesha pia kutofautisha na washindani wako kuonyesha msisimko wa biashara yako. Kwa biashara nyingi, jina mara ni rasilimali ya thamani kubwa sana.
Masharti:
- Mwombaji ni lazima sjaze fomu ya maombi ya kusajili jina la biashara:
- Kwa mtu mmoja mmoja, jaza fomu namba 3
- Kwa ubia, jaza fomu namba 2
- Kwa shirika, jaza fomu namba 8.
- BRELA hufanya utafutaji na uhakiki wa majina
- Huthibitisha au kukataa ombi
- Mwombaji hulipa ada zifuatazo:
- Ada ya maombi y ash.5,000/=
- Ada ya matunzo y ash. 1,000/= (hulipwa kila mwaka)
- Ada ya utafutaji na uhakiki sh. 1,000/=
- Mwombaji hupewa cheti na udondozi atakaotumia mwombajikufungulia akaunti.
- Mwombaji anajaza fomu namba 6
- Baada ya kulipa ada zinazostahili, cheti cha kubadili jina kinatolewa pamoja na udondozi mpya.
- Mwombaji anajaza fomu Nam. BN7 (fomu ya kukoma/kuacha kwa muda)
- Ataambatisha cheti cha usajili halisi
- Atalipa ada ya kukoma/ kuacha kwa muda ya sh. 1,500/=