Msaada: Jinsi ya kununua simu Ebay na kutambua ubora na network yake

Raphael gadau

JF-Expert Member
Jan 17, 2017
1,006
306
Naombeni msaada wa kununua simu mtandaoni kupitia mtandao wa Ebay, hatua za muhimu za kufuata pia hata kuitambua simu Ubora wake hata network yake, unaweza nunua halafu kufika TZ network locked.
 
VISA au Master Card ni kitu Muhimu katika kufanya manunuzi yoyote online
Ukisha weka ccv eBay watakuomba adres na contact zako kisha utaqrick picha ya hiyo sim unayo hita itakupa full information kuhusu hiyo sim au bidhaa unayohitaji
 
Bila visa au master card huwezi nunua??
 
Bila visa au master card huwezi nunua??
Visa au Master Card ni mifumo inayowezesha manunuzi karibu dunia nzima. Hivyo unaeza ukaona simu ya dolla 200 inauzwa USA, kwenye akaunt yako una 1M. Unafanya manunuzi yako huendi forex wala wapi. AU hata uende ulaya ila account yako imewezeshwa kwa pesa zetu za kibongo unaeza fanya manunuzi yako bila shida.
So kwa maisha ya sasa ni muhimu kuwa nayo na iwe imewezeshwa kufanya hizo huduma.
Ila so far kwa sasa ambao naona kadi zao zinafanya hayo manunuzi ni CRDB na NBC
 
Zipo Bank nyingi Tanzania zinamfumo huo tatizo wa TZ ni washamba sana hawatumii Huduma hizi
Mkuu, NMB, EXIM na DTB wanatoa hizo visa/mastercard ila maajabu yake wanakuambia online services hazijakuwa enabled! Ila kwa CRDB na NBC ndio card nimeshawahitumia. CRDB nilitumia England kununua baadhi ya vitu
 
Mimi natumia UBA nafanya manunuzi yangu popote na bidhaa zinanifikia nilikuwa CRDB Huduma zao zikawa za kusuasua bank yao imejaa uswahili mwingi nikajaribu NMB ndio kabisa
Tatizo kubwa la watanzania ni waoga sana wanahisi ukinunua bidhaa online utatapeliwa lakini nikinyume kabisa unaweza kukuta simu Kariakoo inauzwa 600000/ lakini simu hiyo hiyo ukiitafuta eBay unakuta inauzwa $130 mtu anashindwa kununua eBay anunua ya Kariakoo haangali kama kapoteza pesa kizembe tatizo lingine elimu zetu hazina uwezo wakutuandaa kutumia technology katika vitu mbalimbali zinatuandaa kushabikia sio kushindana
 
Kweli kabisa mkuu fakhbros, nakuunga mkono kabisa kuwa wengi tumejawa na woga wa kuthubutu kufanya manunuzi ebay... halafu tunakomaa na kupatana palipojaa majangili wenye pembe....
 
Mimi binafsi ni muoga wa kununua kitu kupitia hiyo mitandao maana zaidi ya mara tatu nikiagiza kinakuja kitu cha quality ya chini tofauti na picha mfano vitu kama viatu, pochi. Huwa mnakwepaje hilo?
 
Mimi natumia UBA nafanya manunuzi yangu popote na bidhaa zinanifikia nilikuwa CRDB Huduma zao zikawa za kusuasua bank yao imejaa uswahili mwingi nikajaribu NMB ndio kabisa
Tatizo kubwa la watanzania ni waoga sana wanahisi ukinunua bidhaa online utatapeliwa lakini nikinyume kabisa unaweza kukuta simu Kariakoo inauzwa 600000/ lakini simu hiyo hiyo ukiitafuta eBay unakuta inauzwa $130 mtu anashindwa kununua eBay anunua ya Kariakoo haangali kama kapoteza pesa kizembe tatizo lingine elimu zetu hazina uwezo wakutuandaa kutumia technology katika vitu mbalimbali zinatuandaa kushabikia sio kushindana
Mkuu samahani kidogo bei hiyo hamna kodi tena na gharama za shipping zinakuwa juu ya nani?
 
Back
Top Bottom