Wadau ninaomba msaada wa jinsi gani naweza kuburn movies nimedownload kutoka youtube zipo vlc na Mp4 nataka nizihamishie kwenye cd; mwenye kujua ni software gani ya kuburn na jinsi gani ya kufanikisha ili niziburn kwa PC yangu anifahamishe tafadhari !
Ndugu jaribu kutafuta program ya convertxtodvd ambayo inconvert videos zako kwenda Video Objects format (VOB) na kuiburn kwenye DVD. DVD yako itakuwa na menu kabisa kama unavyokuta kwenye DVD za bluray na HD Dvd za kununua
Tafuta software inaitwa Total video converter, ukiipata hiyo iinstall, ifungue kisha chukua movie yako uiweke humo itakuonesha unataka kuconvert nini, mf. utaona mp3, mp4, vcd nk.
Chagua vcd baada ya hapo utakuta kuna kitufe kimeandikwa convert iclick, subiri ikishamaliza movie yako itakuwa tayari Vcd.
Fungu burning sofware ya burning, unaweza tumia ashampoo au nero burning, ifungue nero then chagua vcd kisha shuka chini uclick next halafu subiri imalize baada ya hapo Finish, kitu kinakua ok.
Wakuu naomba kufahamishwa,Nimedownload movies zingine ziko kwenye Blue ray nataka nizi burn kwenye DVD,Je ni muhimu kuzi convert kwanza to DVD ndio nizi burn (natumia nero trial version ya two weeks)?
Na kama ni muhimu,je ni FREE CONVERTOR gani ni nzuri na rahisi kutumia?
Naomba msaada wenu wataalam.
Jaribu ku-burn tu kwenda DVD bila convertion, maana software ya Total Video Converter sijaona neno Blue ray, nijuavyo mimi blue ray ni kama DVD tu tofauti yake ni uwezo wake mkubwa wa kuhifadhi data kuizidi DVD.