Msaada jamani kwa wajuzi wa sheria

Msaada jamani kwa wajuzi wa sheria

mafoleni

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2016
Posts
220
Reaction score
371
Nianze moja kwa moja kwenye mada husika.
Ninaishi na mwanamke na tulibahatika kupata mtoto mmoja wa kike. Tumejenga nyumba moja wakati tunaishi nae bila ndoa Ila mimi na huyu mama watoto wangu tumetofautiana kiimani yan yeye muisilam na Mimi ni mkristo nilijitahid sana kufatilia abadili dini lakini ikashindikana.

Sasa mi naona kuishi maisha haya bila kuoana miaka yote ni kitu ambacho kimenishinda ikabidi nimueleze kuwa huu ni wakati wangu wa kuwa na ndoa, na wewe kwa upande wako imeshindikana.

Nilivyomuambia hivyo akahamaki na kuamua kuondoka nyumbani na kwenda kwa dada ake: nimemfuata anakataa kurudi anataka tuuze nyumba ili tugawane ingali Mimi sikumfukuza nyumbani ila nimemwambia nataka ndoa na yeye hawezi kubadili dini.

Vipi kwa upande wa sheria kuhusu mgao kama mwanamke anaamua kuondoka mwenyewe nyumbani?

IKUMBUKWE KUWA HATUKUFUNGA NDOA. ila tumeishi kwa miaka 4.
 
Kishelia ya dunia jinsi watu wanavyo iyendesha kuusu ndoa, kunandoa zaina tatu 3, yani kunandoa yakidini pia kunandoa ya kiserikali pia kunandoa ya kimila, sasa kwanini wewe unaitaji ndoa yakidini pekeyake wakati ndoa zipo zainanyingi ?, au unalengo lakumzulumu mwenzio ?.
 
Ila ikumbukwe Mimi sijamfukuza
 
Kwanza kabisa ufahamu kuwa mwanaume na mwanamke wakiishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi katika hadhi ya mume na mke, basi hiyo ni NDOA,.na hii ni kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania ambayo ilirejewa tena mwaka 2002...hivyo unaweza kupata picha ya kinachoendelea kati yako na mwenzio...

Huo ni muhktasari tuu...
 
Huyo mwanamke umemchoka wala usisingizie ndoa. Ndoa nimakubaliano kati ya mwanamke na mwanaume kuishi kama mke na mume. Hizo nyingine mbwembwe tu.
 
Back
Top Bottom