Wakuu,
Napata Usumbufu kutumia hotspot ya hii iPhone 6, kawaida huwa natumia internet ya simu hii kwenye iPad kwa kutumia hotspot, ninapoconnect inakubali vizuri, usumbufu unakuja ninapoacha kutumia iPad hata kwa dakika mbili tu, nitakapoanza kutumia tena ipad inanibidi kuconnect tena, tena kwa kuzima na kuwasha tena hotspot kwenye simu.
Kabla ya kuwa na simu hii nilikuwa natumia Samsung galaxy S4 haikuwa na tatizo hili, ilikuwa wakati wowote nikiwasha iPad inajiconnect yenyewe kama hotspot kwenye s4 iko ON.
ni jambo hilo tu linaninifanya niimiss Samsung na kuichukia iPhone 6.
Naombeni msaada kama kuna cha kufanya.