Msaada: Htc one M8 haisomi line

Pukudu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
3,157
Reaction score
2,268
Wakuu kama mada inavyojieleza hapo juu, nina simu yangu aina ya Htc one M8 nilikuwa naitumia kama kawaida. Mara ghafla ikawa haisomi line ukiweka line inasema "No Simcard". Nikapeleka kwa fundi wakaiflash haikufaa, wakasema labda ni kile kichuma kinachoshilkilia line walibadilisha lakini simu haikupona. Fundi akaniambia ni tatizo la "software" na wataalam wengi hapa Arusha wameniambia ni tatizo la software bila kusema software ipi na inarekebishwaje .... isipokuwa kuna muuza simu mmoja kaniambia niende Nairobi nako ni kuingia gharama si za msingi.
Naomba kama kuna mjuvi anisaidie niko tayari hata kumtoa "uchakavu" simu ikipona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama waliflash apo ni hardware
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…