Msaada: Gharama za Bugando Hospital

Shimba ya Buyenze

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
181,119
1,094,966
Nina mgonjwa na tumepewa referral kwenda Bugando. Ni wazi tutalazwa huko. Gharama za kulazwa kwa siku ni kiasi gani? Vipi vipimo kama x-ray na vinginevyo? Kumwona daktari bingwa je? Huduma zao zikoje au na penyewe ni mpaka umjue mtu?

Natanguliza shukrani zangu za dhati wapendwa.
 
Hakuna hata mmoja. Dah! Haya bana. Asanteni.
Pole kwa kusubiria jibu ! Bugando wamepandisha sana bei zao kwa hiyo jiandae...kama mgonjwa wako sio wa upasuaji basi jiandae na laki Kama mbili maana kuna elfu 20000 ya file na 150000 ya kulazwa kwa siku nne...kwenye hiyo laki na elfu hamsini kuna 25000 ya vipimo na 25000 na kilichobaki ni laki ya kulazwa kwa siku nne...vipimo na dawa zikizidi hela hiyo itabidi mlipie toka mifukoni kwa hiyo jiandae....Kama ni upasuaji jiandae na laki tatu na elfu hamsini (350000/=)
 
Pole sana kwa kuuguliwa,inabidi ujiandae kisaikolojia maana bugando ni zaidi ya unavyoijua,siku hizi yamebaki majengo ubabaishaji mwingi,vipimo vingi havipatikani bugando mpaka hospitali binafsi,Kama unadaktari labda ungesema mgonjwa anasumbuliwa na tatizo gani ili uweze kupata msaada zaidi maana Bugando ni jipu linahitaji kutumbuliwa
 
Asanteni wapendwa. Mgonjwa wangu alipokelewa na kutibiwa vizuri sana. Vipimo vilifanyika na tatizo likagundulika. Nimeongea naye leo anacheka na wameruhusiwa kurudi nyumbani. Asanteni madaktari bingwa wa Bugando kwa huduma nzuri. Mungu Aendelee kuwabariki na kuitumia mikono yenu iliyobarikiwa ili kuwasaidia binadamu wenzenu wanaoteseka. Amen!
 
Pole sana kwa kuuguliwa,inabidi ujiandae kisaikolojia maana bugando ni zaidi ya unavyoijua,siku hizi yamebaki majengo ubabaishaji mwingi,vipimo vingi havipatikani bugando mpaka hospitali binafsi,Kama unadaktari labda ungesema mgonjwa anasumbuliwa na tatizo gani ili uweze kupata msaada zaidi maana Bugando ni jipu linahitaji kutumbuliwa
Siyo kweli. Tatizo letu Wabongo ni kulaumu na kulalamika. Japo ni mazingira magumu lakini madaktari wetu wanajitahidi sana. Mungu Awabariki! I am eternally grateful!
 
Back
Top Bottom