Sina uhakika kama Humphrey Polepole yumo JF,kama hayupo mtafute Facebook jamaa ni fundi mzuri sana atakusaidia mawazo.
umeoona eeeh lakini yawezekana akawa na ufahamu wa haya makitu!yule wa katiba ?
Betri. Cheki kwanza betri ya gari yako kwenye loose connection na kwenye accummulated carbon na rekebisha hayo. Mara nyingi ni tatizo la betri. Nimesha kesha njiani mimi kwa ajili hiyo!
Angalia na silencer kama ipo sawa, ikiwa chini ukiwasha AC lazima gari izime! Naamini haikuwahi kushushwa ili kubana matumizi ya mafuta kama wanavyofanya wengi wenye masix cylinder!!!! Mafundi watakusaidia
Tatizo kubwa ni cable za plug au plug zenyewe,mimi nilishapata tatizo km hilo.
Mkuu sorry kwa swali la udadisi unaweza nifafanulia hiyo silencer kuwa chini maana yake nini
Silencer = ni urekebishaji wa uwakaji wa injini (Hewa ya Oxygen na petrol zinapoingia kwenye tundu (bore) mlipuko huisukuma Piston ikazungusha unjini nagari kufanya unjini.Mkuu sorry kwa swali la udadisi unaweza nifafanulia hiyo silencer kuwa chini maana yake nini
Wakuu salaam!
Namshukuru Mungu nimefanikiwa kumiliki kausafiri nina funcargo, ila siku za hivi karibuni kuna tatizo ambalo limeanza kusumbua gari langu.Iko hivi gari linapokuwa limepaki na liko ON nikiwasha tu AC huzima, ila nikiliwasha tena na nikawasha AC kuna mawili, AC inaweza ikafanya kazi kama kawaida lakini wakati mwingine bado litazima tena.Ila likiwa kwenye mwendo na nikawasha AC tatizi hili hutokea kwa nadra sana, yaani AC hufanya kazi kama kawaida.Kwa kuongezea nikiswitch tu AC on ghafla kuna mlio wa engine ambao si wa kawaida huibuka (yaani inakuwa kama vile engine inasitasita kufanya kazi au ni kama vile inachezacheza like umeme wa majumbani unavyochezacheza na time hiyo hata dash board huwakawaka na kuzimazima) ni kama vile engine inajaribu kupambana na mzigo mzito ambao inakuwa imetwishwa ghafla kwa AC kuwa on ! vile vile taa ya cheki engine huwaka ingawa baadae huzima.
Naomba kwa anayeelewa anieleweshe hasa tatizo laweza kuwa nini, maana mafundi kadhaa nilioongea nao kila mtu anakuja na la kwake!
Napenda angalau kuwa na clue/idea maana kibongobongo mafundi wengine si waaminifu wanaweza kula pesa zangu ilihali tatizo laendelea kama kawa.
Nashukuru sana kwa mawazo mbalimbali yatakayojitokeza.
Silencer = ni urekebishaji wa uwakaji wa injini (Hewa ya Oxygen na petrol zinapoingia kwenye tundu (bore) mlipuko huisukuma Piston ikazungusha unjini nagari kufanya unjini.
km kimojawapo ya Hewa au petrol kikapungua injini hukosa nguvu na kuzima au ikamaliza petrol yako km utazidisha.
Ndio maana ukiiwasha AC peke yake inashindwa wakati gari limesimama kwani unatumia Betri Ndogo ya Volt 12 lkn ni N40
- Hizo gari hutumia Fan-belt inayozungushwa na Pull ya injini na pia kuna Fan ingine ipo katika Rejeta
- Kwa hiyo huhitajika nguvu ya ziada kuitembeza injini kwani humaliza petrol
- na mara nyingi humaliza nguvu ya Betri km utawasha pia na taa na music
HUENDA ikawa na tatizo la Betri kutoa moto mdogo na altenator kuzidiwa nguvu
Belt kumaliza muda wake au Fan ya AC kutokufanya kazi
wASILIANA na mafundi wa umeme wa gari au AC
mshana jr nakuomba uachiliwe mapema unahitajuka huku AC inamsumbua Member
Ahsante sana mkuu Brondo Mungu akubariki mara dufu kwa msaada wako! na je hiyo idle control ni nini hasa!mkuu hapa una tatizo kwenye AC system, kwa kifupi AC compressor ikianza kufanya kazi[ukiwasha AC] inaleta mzigo mkubwa kwenye engine hivyo kwenye hali ya kawaida engine inajiongeza rpm[ mara nyingi kutoka 600/700-1000/1200 revolution per minute] ili kuipa engine nguvu zaidi ya kuhimili mzigo wa ac compressor.
inaonesha hapa gari yako haijiongezi rpm ukiwasha AC INABAKI ile ile 600/700 rpm hivyo engine kushindwa kubeba mzigo wa ziada kutoka kwa ac compressor,gari itazima. ukiwa kwenye mwendo haizimi kwasababu ukikanyaga mafuta rpm itakuwa juu ya 1500 kwa hali ya kawaida.
ninachokushauri nenda kwa mafundi wa AC waangalie system nzima kwenye gari yako,inawezekana compressor imeanza kufa au tatizo lingine kwenye idle control.
Ahsante sana mkuu Brondo Mungu akubariki mara dufu kwa msaada wako! na je hiyo idle control ni nini hasa!