Mojawapo Kigezo cha kujua kuwa SACCOS unayotaka kujiunga nayo kuwa sustainable 'endelevu', ni kuwa na wanachama wengi 'hai' wanaopata huduma. SACCOS yenye wanachama wengi hai kwa kawaida lazima hata mtaji wake utakuwa ni mkubwa kwa kuwa watu watakuwa wanafanya savings kwa kiasi kikubwa na watakuwa wanakopa kwa kiasi kikubwa pia,hivyo SACCOS kupata kipato kikubwa kupitia riba inayopatikana kupitia marejesho wanayoyafanya.
Ukiona unaenda SACCOS unakuta kuna movement chache za wateja, lazima itakuwa haipo vizuri sana,ukiona unaenda SACCOS kutaka kukopa unaambiwa uje baada ya miezi miwili au zaidi,ujue hawana mtaji wa kutosha.
Taratibu za kuwa mwanachama ni kwenda kwenye Ofisi za SACCOS husika,watakupa taratibu zote ikiwemo kulipia kuwa mwanachama, kununua Hisa,n.k.
Ukitaka kukopa lazima uweke akiba na utakopeshwa si zaidi ya mara tatu ya akiba yako, Mfano Ukiwa na Akiba ya milioni moja, utakopesha milioni tatu kwa riba watakayokuelekeza na muda wa marejesho utakaoelekezwa,wengine wataongezea mkuu.