Msaada: Chuo chao kimefungiwa, je atapataje cheti?

Msaada: Chuo chao kimefungiwa, je atapataje cheti?

Rahma Nyusi

Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
73
Reaction score
9
Habarini jf.
Nina mdogo wangu amemaliza certificate royal college mwaka jana ila mpaka sasa hajapata cheti. Nimejaribu kufatilia chuoni mara kadhaa wana sema vyeti bado havija sainiwa nimeuliza vitatoka lini kila siku wananipiga calender.

Siku za hivi karibuni nimefatilia kuna dogo alikuwa anasoma pale diploma amesema wamehamishiwa st Joseph kwa course ya social work na wale wa jornalism wamehamishiwa DSJ.

Sasa naomba kuuliza wana member je, kwa mdogo wangu ambaye amemaliza hapo mwaka jana na cheti hawakutoa kwa madai ya vyeti kutokusainiwa anawezaje kupata cheti?Maana chuoni nimekwenda mara kadhaa hawanipi majibu ya kuridhisha zaidi ya kunipiga calender.
 
Kwa wale waliomaliza kabla ni haki yao kupata cheti..
Kama wanagoma kutoa cheti bila sababu wapeleke kwenye mamlaka husika NACTE au mahakamani kabsa..
Vipi wenzake walishapata?
 
Kwanza pole sana kwa yanayokukuta na yanayomkuta dogo. nikiwa mdau wa elimu, naweza kuelewa kile unachopitia.

Jambo la pili, fuatilia kuona kama na wengine wako katika condition hiyo ama laa. maana hawa madogo zetu sometimes huwa hawaeleweki. Usikute dogo hakumaliza shule na alikula ada na wadau hapo chuoni ndo maana wanazingua. ama laa, basi ungaenni na wahanga wengine mlitatue kwa pamoja. UMOJA NI NGUVU. SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU

Tatu, kuna vyombo vinavyo regulate masuala ya elimu, na kupata cheti ni haki hako. NACTE hapa ndo inahusika.

Fuatilia huko. Ikishindikana, wapeleke mahakamani
 
kwanza pole sana kwa yanayokukuta na yanayomkuta dogo. nikiwa mdau wa elimu, naweza kuelewa kile unachopitia.
Jambo la pili, fuatilia kuona kama na wengine wako katika condition hiyo ama laa. maana hawa madogo zetu sometimes huwa hawaeleweki. usikute dogo hakumaliza shule na alikula ada na wadau hapo chuoni ndo maana wanazingua. ama laa, basi ungaenni na wahanga wengine mlitatue kwa pamoja. UMOJA NI NGUVU. SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU
Tatu, kuna vyombo vinavyo regulate masuala ya elimu, na kupata cheti ni haki hako. NACTE hapa ndo inahusika.
Fuatilia huko. Ikishindikana, wapeleke mahakamani
Ahsante sana kwa kunifariji.Dogo chuo aliudhuria vizuri na nimeona kwenye system yao matokeo yake yako vizuri ila cheti tatizo kila siku wananipiga calender
 
Back
Top Bottom