Msaada-cheti cha kuzaliwa.

Too face

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
223
199
Wakuu naomba kujua gharama za kuchukua cheti cha kuzaliwa RITA kwa mtoto aliyezaliwa mkoani ni sh ngapi kwa sasa,na inachukua muda gani kukipata?asanteni.
 
Nilikuwa Hapo Rita Mwezi Uliopita Huduma Ni Mzuri
Kuna Gharama Chache Halafu Ndani Ya Wiki 2 Hadi 3
UtakuwA Umepewa Cheti

Kuna Ada Ya Upekuzi 1500/- Unalipa Kwa Mpesa/Tigo/Airtel Yaani Kuangalia Kama Kweli Kazaliwa Huko Unakosema Wewe.

Awe Na Viambatanisho Kimojawapo Kati Ya Hivi
Tangazo La Kuzaliwa Mtoto
Cheti Cha Ubatizo
Kadi Ya Kliniki

Kuna Form Utajaza Halafu Utalipa 3500/-
Baada Ya Hapo Ni Wiki Moja
Mimi Nimepata Hicho Cheti Kwa Haraka Bila Kuombwa Chochote Zaidi Ya Hayo Mahitaji.
 
Back
Top Bottom