Mkuu kwanza pata michoro (both Architectural and structural) na iwe imegongwa mihuri ya registered engineer (kwa structural drawings). Kisha nenda nayo pale Temeke manispaa. Gharama yake haizidi shilingi za kitanzania elfu arobaini na tano tu. Ila kama kuna vikorombwezo vingine mfano, ukuta (fence), servant quarter n.k gharama zinaongezeka kidogo. Hawa jamaa hufanya vikao vyao mara moja kwa kila miezi miatatu kutoa vibali isipokuwa kama kuna dharura ambapo mwombaji inabidi alipe kama milioni 2. Kwahiyo fanya mapema waweza kubahatisha ukakuta kikao kiko karibu kufanyika.