Msaada: Binti anamtafuta baba yake

Msaada: Binti anamtafuta baba yake

Easymutant

R I P
Joined
Jun 3, 2010
Posts
2,564
Reaction score
1,135
Heshima kwenu!

Naomba kuwasilisha ni Dada ambaye anamtafuta baba yake, kwa ufupi mtoto hajawahi kumwona baba yake.

Mtoto anaishi Nairobi na anasema anamtafuta amjue baba yeke,si kwa lengo la kutaka msaada wa kifedha kutoka kwa baba ila anajisikia vibaya kuishi bila kumjua baba.

Anaendesha maisha yake vizuri tu na kwa bahati mbaya mama yake ameshatangulia mbele za haki.

Baba anaitwa Ramadhani Mangile aliwahi kuambiwa anafanya kazi Dar-es-salaam.

Haijajulikana ni kampuni gani alikuwa akifanyia lakini kazi yake ni dereva wa maroli.

*He was a short man and he used to deal with trellas butt he was staying in dar es laam town*

Dada alifanikiwa kutoa box number pekee ya kampuni alikokuwa anafanyia kazi baba yake Box number 67696 Dar-es-salaam.

Baba ni Mtanzania anatokea sehemu inaitwa MALOLO (sijawahi kupasikia na sipajui).

Ninaamini humu ndani atapata msaada wa kumpata baba yake.

(mwenye kuweza kutoa directives za huyu dada kumpata baba yake tafadhali unaweza kushare privately) PM.

Asanteni
 
Nenda posta ulizia ilo box kwa miaka hiyo lilimilikiwa na nani, mkiipata labda record zake bado zitakuwepo.
 
Amtaje mama yake jina full na maeneo aliyokuwa anakaa,si unajua sisi wa malori kila kituo ni nyumbani?
 
IPO malolo nyingine maeneo ya mchinga no 2, lindi ji mbo lililokuwa LA mudhihiri
 
Malolo ninayo ifahamu Mimi ipo mpakani mwa Iringa na Morogoro;yaani ukitoka Dar unafika mpaka Ruaha Mbuyuni! Kabla hujavuka daraja,unapinda kulia au ukiulizia wenyeji wa hapo watakuonyesha hicho kijiji kilipo: kijiji hiki ni maarufu kwa kilimo cha vitunguu na matikiti maji!!
 
Hawezi kumpata kwani information hazijatimia! hasa jina la mama yake! ukoo wa baba yake! alizaliwa mwaka gani, maeneo gani,
 
Dereva wa malori kwa miaka hiyo!!! Yupo hai kweli? Samahani ila nimeenda mbali sana kwa kuwa hawa madereza wengi wa safari za mbali ni marehemu na wengi walikufa kwa UKIMWI. Mungu asaidie tu akute yuko hai aone aibu ya kusambaza mbegu bila kuzimwagilia. Ni aibu sana unazaa then unasahau kuwa wewe ni mzazi. Tunatesa watoto sana kwa hili.
 
Kuna malolo moro na singida, ongeza info zaidi
 
njia rahisi ni kwenda posta kujua mmiliki wa anwani ya posta ukishapata nenda kampuni husika kazi itakuwa imekwisha
 
Dereva wa malori kwa miaka hiyo!!! Yupo hai kweli? Samahani ila nimeenda mbali sana kwa kuwa hawa madereza wengi wa safari za mbali ni marehemu na wengi walikufa kwa UKIMWI. Mungu asaidie tu akute yuko hai aone aibu ya kusambaza mbegu bila kuzimwagilia. Ni aibu sana unazaa then unasahau kuwa wewe ni mzazi. Tunatesa watoto sana kwa hili.
duh......
 
Back
Top Bottom