WENYELE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,432
- 1,441
Ndugu madaktari na Wauguzi,habari zenu,poleni na majukumu ya ujenzi wa taifa letu hili.Naomba msaada wenu wa hali na mali kuhusu nifanyaje kuhusu bibi yangu.
Bibi yangu ni mzee karibia zaidi ya miaka 90 ila bado ana nguvu japo kwa sasa zinaisha kulingana na magonjwa yanayomzonga. Anasumbuliwa na kufua kubana na kupumua kwa shida,miguu kuvimba na tumbo la mara kwa mara.Bibi yangu anaishi kijijini na haya maradhi yote yanatokea ndugu na jamaa wanadai kalogwa,hapa juzi kati nimeshikiniza kumpeleka hospital na nikatoa hela yangu ila ndugu na watoto wake (mashangazi na ba mkubwa waligoma) cha ajabu akatafutiwa mganga eti ndo anamtibu kienyeji tena kwa gharama kubwa tu..
Sasa wanasema anaumwa "Mang'ondi' sjui ni ugonjwa gani kwa kiswahili lakini kwa wasukuma wenzangu hasa Bariadi wanaweza wakanisaidia kutafasri 'Mang'ondi' ni nini....kiukweli hii tiba sina imani nayo...wanasema ana uvimbe haja kubwa na ndogo na kumtibu wanatumia dawa za kienyeji kumsugua....sasa bibi nguvu hana anashindwa hata kusimama ama kukakaa.Jana niligombana sana na ndugu kuhusu tiba hii,wakakubali leo wangempeleka hospitali na hela nikatoa cha kusikitisha hawajampeleka na bibi anaendelea kuteketea tu...Mi wakuu niko mbali sana na nyumbani sasa kila msaada wa mawazo nikitoa ndugu hawataki ila wanataka nitume hela tu.Naomba msaada ufutao
1.Bibi anakosa ham ya kula je ni chakula gani kwa mtu mzee wa zaidi ya miaka 95 inashauriwa ale? Walikua wanampa soda na biscuit km chakula chake ila nimekataa nimewaambia wampe matunda na mboga za majani kwa wingi,je nyama pia inaruhusiwa yeye kula..ila bahati mbaya hana meno
2.Ni tiba ipi anaweza akatumia kwa matatizo yanayomsumbua kwa sasa yaani kupumua kwa shida akitembea,tumbo na miguu kuvimba.
3.Je akiwa.nyumbani mitishamba ngani anaweza kuitumia ili imsaidie?Nyumbani kuna kwetu kuna Mlonge,alovera,Mdalasini na Mwarobaini
Natanguliza shukrani zangu kwenu