Najaribu! unatakiwa uwe na chumba kikubwa chenye partion mbili,moja inakuwa kama store ya dawa...sakafu ya tiles na makabati ya aluminium,haya hayabebi uchafu sana na rahisi kusafisha..Kutoka kwenye duka lako hakikisha hakuna duka lingine umbali wa chini ya mita 300..ukishapata eneo lako la biashara nenda kamuone mfamasia wa wilaya atakuja na timu yake kukagua kisha utapewa go ahead..Utahitaji leseni ya biashara na kibali kutoka TFDA ambayo ni mamlaka ya chakula na dawa...Mtaji inategemea na ukubwa wa duka unalotaka,kuanzia milioni 2 unaweza pata dawa za kuanzia hiyo ni nje ya gharama jengo,makabati,na process ya vibali