MSAADA: Basi la abiria zuri la Mbeya hadi Mwanza

HISTAMINE

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2014
Posts
649
Reaction score
1,573
Habari wakuu, naomba kujua ni gari gani zuri (kwa maana ya kufika kwa wakati na huduma nzuri) la safari za Mbeya hadi Mwanza. Sipendi kuunga unga safari kwa maana ya kuishia Dom then niunganishe, hapana, nataka la moja kwa moja. Haijalishi kama litakuwa ni luxury au la, nnachotaka ni safari ya moja kwa moja na isiyokuwa na ubabaishaji kama vile mnasafiri linaharibika kila baada ya lisaa, au mnaenda mwendo wa kumsindikiza bi harusi, hiyo sitaki.
Sijasafiri njia hiyo muda mrefu ndio maana nimekuja hapa nipate uhakika wa basi zuri la abiria kabla sijaianza safari hivi karibuni. Ahsanteni.
 
Hakuna basi luxury kwa safari za mwanza to mbeya...basi ziko mbili tu isamilo na premier line exp...kuhusu kuwahu kufika ni kuwa ukitoka mbeya saa kumi na mbili asubuhi utafika mwanza saa kumi alfajiri siku ya pili
 
Isamilo ndo angalau utawahi kufika
 
Panda best line
Hutojutia
Hiyo haipo saivi. Basi zipo mbili Isamilo na Premier na Turu best yakuishi Singida.
Best line ilishabadilishwa jina now inaitwa Serengeti line inaenda Dar to Mwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…