HISTAMINE
JF-Expert Member
- Nov 26, 2014
- 581
- 1,389
Habari wakuu, naomba kujua ni gari gani zuri (kwa maana ya kufika kwa wakati na huduma nzuri) la safari za Mbeya hadi Mwanza. Sipendi kuunga unga safari kwa maana ya kuishia Dom then niunganishe, hapana, nataka la moja kwa moja. Haijalishi kama litakuwa ni luxury au la, nnachotaka ni safari ya moja kwa moja na isiyokuwa na ubabaishaji kama vile mnasafiri linaharibika kila baada ya lisaa, au mnaenda mwendo wa kumsindikiza bi harusi, hiyo sitaki.
Sijasafiri njia hiyo muda mrefu ndio maana nimekuja hapa nipate uhakika wa basi zuri la abiria kabla sijaianza safari hivi karibuni. Ahsanteni.
Sijasafiri njia hiyo muda mrefu ndio maana nimekuja hapa nipate uhakika wa basi zuri la abiria kabla sijaianza safari hivi karibuni. Ahsanteni.