Msaada: Anayepafahamu Shighatini, Ugweno

Msaada: Anayepafahamu Shighatini, Ugweno

Asee kwaiyo kumbe miundombinu ni mibovu kule.
Eti ni ka mji ka ovyo hivyo.
Mbona ni hatari hii sasa
Huyo amefika Ugweno ya miaka hiyoo! Kiufupi sasa hivi ni lami kuanzia Mwanga mpaka Usangi,Pia kuelekea Ugweno ndani ndani lami inaishia Msangeni na kunapitika mwaka mzima.Vyakula bei nafuu sana.Kwa mfanyakazi uta enjoy sana.Mimi ndio nyumbani na ninapafahamu Ugweno na Usangi yote.
 
Asee kwaiyo kumbe miundombinu ni mibovu kule.
Eti ni ka mji ka ovyo hivyo.
Mbona ni hatari hii sasa
Watu wanaangalia potentiql ya eneo upande wa fursa sio kutafuta barabara ya kupitushia vitz yako
 
Asee kwaiyo kumbe miundombinu ni mibovu kule.
Eti ni ka mji ka ovyo hivyo.
Mbona ni hatari hii sasa
Anakudanganya. Nyumbani Kwetu sisi ni ugweno,nimeishi na ninapafahamu vilivyo.

Kuna hali ya hewa iliyopoa,ya baridi kama moshi/arusha hivi.

Kuna barabara ya lami kutoka Mwanga mjini mpaka huko milimani. Barabara ya lami inafika mpaka hapo Shighatini.

Wenyeji ni mchanganyiko wa Waislam na Wakristo(Walutheri)

Kama unaswali lingine uliza.
 
Salam wakuu,
Anayefahamu shighatini na maisha ya pale kiujumla kwa mtu anayetaka kuhamia/ , jamii ya pale ipoje kiujumla
Tanzania nimeizunguka.
Shighatini napajua sana.
Kijana wangu ni ni Daktari pale Usangi ni mbele kidogo ya Shighatini.

Kiufupi Shighatini kwa historia yake ni sehemu nzuri sana na ina watu wenye maendeleo makubwa Sana.
Nilioma Ghorofa kubwa mlimani jirani nikaambiwa ni ya mkubwa Fulani huko kwenye taasisi Fulani kubwa.

Kuna Lami nzuri kabisa na mabasi ya kwenda Moshi,Arusha ,Dar es salam yanapita kwenye kijiji hicho kielekea Usangi .
Usangi ina watu mashuhuri na wasomi wengi sana na kuna maendeleo makubwa sana mana kuna Pia hospitali kubwa.
Nilionyeshwa nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya ,Waziri mstaafu na Mbunge Mh.Magembe,Aliyekua Naibu Katibu Mkuu wa UN Dr.Asharose Migiro.Waziri wa kwanza mstaafu wa Tamisemi Peter Kisumo,IGP Mstaafu Mgaya,Usangi ni kijijini lakini nilona zaidi ya majengo ya ghorofa kumi ya maana na majumba mengi sana ya maana.
Kuna makanisa mengi makubwa na ya kisisa sana.
Shighatini niliambiwa ndio aliposhukia Mmisionari wa kwanza huko Usangi na kuna mlima mrefu ambao alizikwa maeneo hayo na makaburi yako karibu na barabara yaliyozikwa wajerumani waliokua wanafanya kazi ya misheni.
Shighati sikuona msikiti eneo la karibu.
Ila niliona kibao cha Shule ya Msingi na sekondari na Kanisa la KKKT. Roma sikuona wala sabato japo nafikiri yapo lakini sikuyaona hilo eneo.

Nilibahatika pia kwenda mpaka Kijiji kingine Unapopita njia panda ambalo napo kuna Hospitali kubwa.
Kuna Hali ya hewa nzuri. Nilishtka kuona jengo la ghorofa zaidi ya Tano nikaambiwa ni nyumbani kwa mtu.
Huko kuna misikiti mikubwa sana na makanisa makubwa kuliko hata ya mjini. Kuna Kanisa moja la mviringo ni kubwa sana nadanai linauwezo wa kubena watu 2000 na zaidi.
Eneo hilo sijakumbuka jina lake labda niulize lakini napo pia kuna barabara ya lami japo naona bado inatengenezwa haikwemda mbali sana na pia kuna Ziwa la maji lipo karibu na barabara linapendeza sana.

Kama unasafari ya huko utainjoi sana

Huwezi ukapalinganisha na Lindi, kama mtu mmoja wapo alivyocomment.
Lindi napo napafahamu vizuri mpaka Ngapa wanapolima Minazi huko kwa kina Mh.Nape na Ruangwa kwa Mh. PM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom