Umri wangu 30 ni mwanamke napendwa na huyu kaka lakini kunioa hataki ,tatizo ni mm sina uzazi .
Anataka kuoa mwanamke mwingine lakini kiniacha hataki na kuwa mchepuko sitaki .
Naomba ushauri wenu wauungwana
Hapo yakupasa uwe mvumilivu mana hata utakaempata ukimwambia hali yako lazima atakuwa na nyumba ndogo tu..Pole sana mana najua muda mwingine nadhani huwa unawaza mpaka wataka kumkufuru Mungu wako ila ndo mitihani inayomkabili binadamu yakupasa uwe na moyo mgumu fanya upate mtoto hata wa kum asili au hata wa ndugu yako ukamlea na kumhudumia vizuri kama mwanao na wewe utajiona mwenye thamani kama wengine.
Polee sana,tafuta man ambaye ana tatizo kama lako muyajenge maana kwa inavoonekana pengine huyo man hataki kukuoa kwa sababu ya tatizo ilo ulilonalo lakini anahofia kukwambia ukweli ndo mana anakuzungusha hivo.