Msaada: Amepandikiziwa HIV baada ya kukataa kuwa na mahusiano ya kimapenzi

coco beby

Member
Dec 18, 2015
55
107
Wakuu rafiki yangu hivi ninavyoongea ni mtu wa mawazo muda wote . Naombeni ushauri wenu kuna jamaa alimtongoza alipokataa akamwambia atamkomoa. Atafanya awezalo ili asiwe na mwanaume yoyote kimapenzi

Na huyo jamaa Baba yake ni mganga wa kienyeji kwa ufupi ni watu wanaotumia nguvu za giza. Kinachotokea ni kwamba binti alianza kupokea sms za vitisho na akaambiwa awahi hospital akapime Afya yake Kwani mume anaye ishi naye ni mgojwa wa HIV ,

Rafiki yangu huyo ndipo alipokuja kunilalamikia kwa nini iwe hivyo ndipo nilipomshauri waende hospital wakajue afya zao lakini alikataa na kuniambia wametoka kupima miezi mitatu iliyoisha yeye na huyo shemeji ambaye ndiye mumewe.

Sms zikawa zinaendelea kutumwa na no isiyojulikana zikisisitiza aende hospital mumewe ameugua, mwisho ikabidi binti amsihi mumewe wakaenda waliyoyakuta huko ni kwamba mwanaume mzima mwanamke ndio vipimo vinaonyesha positive.

Binti anasema hajawai kuwa na mahusiano kiholela kwa ufupi anasema hajawai kufanya sex na mwanaume ambaye hajui afya yake pia kabla hajaolewa alipima afya na mumewe .walipima afya zao mara 2. Vipimo vipo vizuri na ndio maana wakafunga ndoa.

Kwa mujibu wake akaamua kwenda kwa mganga kijijini kwao kuangalia nini tatizo ndio kufahamu yule mwanaume aliyemkataa ndiye aliyempandikizia HIV

Sasa issue ni kwamba binti amehangaika sana kwa wataalam lakini mwisho hali bado ile ile ipo kwake tu. Nikimuhoji au kumuuliza kama alijichoma na vitu vya incha kali anasema hapana.

Na huyo jamaaa sasa amejionyesha wazi anasema akitaka apone hilo tatizo awe nae kimapenzi sasa binti hataki kuwa nae maana binti ameshaolewa.

Nawasilisha. Naombeni mawazo yenu katika hili jambo hili ni swala serious kama huna cha kuchangia dharau kejeli si mahala pake . rafiki yangu yupo katika wakati mgumu sana.
 
sasa tunatoa ushauri gani na yeye anaona waganga ndio watakaomsaidia?

la msingi aachane na fikra potovu na kuomba Mungu amuepushe na hilo janga. Yesu pekee ndo suluhisho ila kwanza atoe fikra za kusaidiwa na wanadamu wenzake (waganga)

hilo tu ndilo ningeweza kumshauri.
 
Maisha ni mfululizo wa matatizo na chembe ndogo za furaha.mwambie asihangaike kwa waganga atapoteza ela tu.kikubwa apo kumrudia Mungu wake
 
Mambo ya waganga wa kienyeji na digital wapi na wapi? Huku sisi tupo ulimwengu wa ki-digital, labda ukaombe ushauri ulimwengu wa giza. Akiendelea kwenda kwa waganga wa kienyeji, atapanda cheo muda si mrefu.
 
Uganga hauwezi kupandikiza hivyo vitu cha msingi aachane na mawazo ya kichawi, hicho ni kiini macho
 
Kama ni kweli mwambie aende Kanisani,,, aokoke,,, ataombewa na kupona kabisa. Hayo ni mapepo tu,,, yakimtoka,, anakuwa mzima
 
Amepandikiziwa HIV.!?
Aaende kwa Gwajima akaombewe
Au atafute Mganga anaemshinda huyo dogo anaemtaka nguvu,
Akiona vigumu akubali ombi la jamaa kwa ataondoka nayo.!?
 
Mwambie anywe ARV tu....mpk leo mtu unaamini mambo ya kishirikina kwny ukimwi
 
Wakuu rafiki yangu hivi ninavyoongea ni mtu wa mawazo muda wote . Naombeni ushauri wenu kuna jamaa alimtongoza alipokataa akamwambia atamkomoa. Atafanya awezalo ili asiwe na mwanaume yoyote kimapenzi

Na huyo jamaa Baba yake ni mganga wa kienyeji kwa ufupi ni watu wanaotumia nguvu za giza. Kinachotokea ni kwamba binti alianza kupokea sms za vitisho na akaambiwa awahi hospital akapime Afya yake Kwani mume anaye ishi naye ni mgojwa wa HIV ,

Rafiki yangu huyo ndipo alipokuja kunilalamikia kwa nini iwe hivyo ndipo nilipomshauri waende hospital wakajue afya zao lakini alikataa na kuniambia wametoka kupima miezi mitatu iliyoisha yeye na huyo shemeji ambaye ndiye mumewe.

Sms zikawa zinaendelea kutumwa na no isiyojulikana zikisisitiza aende hospital mumewe ameugua, mwisho ikabidi binti amsihi mumewe wakaenda waliyoyakuta huko ni kwamba mwanaume mzima mwanamke ndio vipimo vinaonyesha positive.

Binti anasema hajawai kuwa na mahusiano kiholela kwa ufupi anasema hajawai kufanya sex na mwanaume ambaye hajui afya yake pia kabla hajaolewa alipima afya na mumewe .walipima afya zao mara 2. Vipimo vipo vizuri na ndio maana wakafunga ndoa.

Kwa mujibu wake akaamua kwenda kwa mganga kijijini kwao kuangalia nini tatizo ndio kufahamu yule mwanaume aliyemkataa ndiye aliyempandikizia HIV

Sasa issue ni kwamba binti amehangaika sana kwa wataalam lakini mwisho hali bado ile ile ipo kwake tu. Nikimuhoji au kumuuliza kama alijichoma na vitu vya incha kali anasema hapana.

Na huyo jamaaa sasa amejionyesha wazi anasema akitaka apone hilo tatizo awe nae kimapenzi sasa binti hataki kuwa nae maana binti ameshaolewa.

Nawasilisha. Naombeni mawazo yenu katika hili jambo hili ni swala serious kama huna cha kuchangia dharau kejeli si mahala pake . rafiki yangu yupo katika wakati mgumu sana.
Kama aliendelea kuwa na mumewe na hakumwambukiza basi huo sio ukimwi ni kiini macho yeye atulie afanye mambo mengine huo hauna madhara ata kidogo
 
Mmm,jamani ivi hii mabo inawezekana? mbona kama naona vitu vya ajabu yani ukapimwe HIV hospital unaonekana Positive lakini sio positive kwenye mwili siamini sanaa,lakini kwa mwenyezi mungu hakuna kubwa,ebu mwambie aende akanunue vipimo ajipime mwenyewe nyumbani may be huyo jamaa anamfatilia kila anapokwenda hospital uenda alitoa hela wampe majibu hayo,sasa akachukue kipimo ajipme mwenyewe...
 
Muambie aende akaombewe ila isije kuwa ana Ukimwi kweli ila hataki kuukubali ukweli, anywe tu dawa asije akafariki mapema
 
Back
Top Bottom