Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)Limewataka wale wote walikabidhiwa hati za viwanja katika eneo la Safari City lililopo kata ya Mateves nje kidogo ya jiji la Arusha kuhakikisha wanaendeleza maeneo yao ili kuruhusu huduma muhimu za umeme na maji ziweze kusogezwa katika mji huo mpya .
Akizungumza mapema leo Nov 15,katika hafla ya makabidhiano ya Hati ya umiliki wa eneo na kibali cha ujenzi kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira(AUWSA) iliyofanyika katika eneo hilo LA Safari City lililopo Burka katika kata ya Matevesi,jijini Arusha, Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa,Dkt.Maulidi Banyani amesema kuwa shirika hilo katika kuhakikisha linafikia malengo ya kusogeza huduma zake kwa jamii ya watanzania wa vipato vyote ,limeanzisha mji huo kwa lengo la kuuza viwanja na nyumba kwa bei nafuu ili kusigeza huduma muhimu kwa jamii na kupunguza msongamano mjini
Ameeleza kuwa limeingia makubaliano na AUWSA na kuwapatia eneo lenye ukubwa wa squaremita elfu 13 kwablengo la kujenga ofisi kuu ya kanda,Karakana,Bohari na Kituo cha Taarifa za mita hatua hiyo itasaidia kupunguza tatizo la maji katika eneo hilo baada ya mamlaka hiyo kuonyesha nia ya kusogeza huduma hiyo kupitia mradi huo.
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa AUWSA Mhandisi Humphrey Mwiyombela amelishukuru shirika la nyumba kwa kuwapatia eneo hilo nakuahidi kujenga jengo lenye ukubwa wa ghorofa sita litakalotumika kama ofisi kuu ya kanda ambalo litafungwa mitambo maalumu ya kupokea taarifa za mbali mbali katika mtandao wao wa huduma za maji.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Auwsa Dkt Richard Masika amesema kuwa ujio wa mamlaka ya maji katika eneo hilo la safari City litakuwa ni mkombozi kwa jamii inayozunguka katika eneo hilo na maeneo ya jirani kwa kuwa kutakuwa na mtandao mabomba ya maji wenye teknolojia mpya na hivyo kuondoa tatizo la maji katika eneo hilo na kuwa kitovu cha sehemu ya mradi wa billion 520 kwa kuboresha mawasiliano.
Ends...........
[https://lh3]