Mrithi wa Marehemu Sheikh YAHYA na utabiri mwaka 2012

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
HassanYahya2.jpg

Kila mwaka aliyekuwa mnajimu na mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein alikuwa akifanya utabiri. Mwaka huu Januari 13, mrithi wa kazi zake Maalim Hassan Yahya Hussein amechukua nafasi yake.


Mwaka huu wa 2012 umeanzia siku ya Jumapili, siku hii inatawaliwa na Sayari ya Jua ambayo nyota yake ni moja tu nayo ni nyota ya Simba.

Sayari hii inahusika na, kufanyiana kiburi, kutumia nguvu, ufahari, mambo yote yanayohusiana na Siasa, udereva, ufundi wa mambo ya moto na magari

Tarehe 20/5/2012 ambayo pia itakuwa siku ya Jumapili Jua litapatwa kiasi (Partial Eclipse) kwa mara ya kwanza na kupatwa huku kwa jua kutaonekana kwa upana wa kati ya kilometa 240 na 300 na sehemu zitakazohusika ni Asia Mashariki, Kaskazini mwa bahari ya Pacific na Magharibi ya Marekani.

Tokyo (Japani) ambayo iko kilometa 10 mwa mstari wa kati itashuhudia kupatwa huku kwa dakika 5 na sekunde 26.
Mwisho wa Mwaka huu tarehe 13/11/2012 ambayo itakuwa siku ya Jumatano ambayo inatawaliwa na sayari Mercury jua litapatwa kamili (Total Eclipse) watu wanaoishi Australia na Bahari ya Pacific ndio watakaokumbwa na kiza cha kupatwa na jua.

Kwa sababu huu mwaka umeanzia na siku ya Jumapili na siku hiyo inatawaliwa na sayari ya Jua, hatari za kupatwa huku zitaikumba Dunia moja kwa moja.

Mwaka huu una namba 12 (2012) ambayo kinyota inaashiria, uadui wa kisiasa na kijamii, watu kulipizana visasi na upinzani kupata nguvu, wanyonge kudai haki zao kwa nguvu na mafanikio ya wataliwa dhidi ya watawala.

Vile vile inaashiria kutokea kwa vimbunga, kusikika sana kwa habari za Waandishi au Waandishi kupata madaraka makubwa katika siasa.

Pia ni mwaka ambao kutazuka Moto sehemu mbalimbali duniani na kuleta madhara makubwa na hiyo inaashiria kuzuka kwa magomvi baina ya viongozi wa kisiasa na wananchi.

Pamoja na hayo tutasikia habari za kutokea matetemeko ya ardhi yatakayoleta madhara makubwa, Wasanii kupata kwa kuchaguliwa au kuteuliwa kushika nafasi za kisiasa na kutokea kashfa kubwa kwa viongozi zitakazohusiana na masuala ya fedha au mambo ya ufisadi au wizi mkubwa utakaoshitua watu.

Kutokana na hayo:-

Natabiri kutokea shida kubwa za Majanga ya Asili na kuongezeka kwa maradhi au kufumuka maradhi yasiyojulikana na kuiletea Dunia wasiwasi mkubwa.
Natabiri, Uadui mkubwa kutokea kati ya viongozi wa nchi na wananchi kwa ujumla na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na viongozi kuvuliwa madaraka.
Natabiri kutokea vifo vya Mahakimu na Majaji na Wanasheria maarufu katika nchi za Mashariki, Tanzania ikiwemo
Natabiri kutokea vifo vya Mawaziri na Wizara zao kupatwa na matatizo.
Natabiri Kutokea kwa Njaa kali kutokana na Jua kuwa kali na ukame kukumba nchi.
Natabiri tutasikika habari za wanawake kuuwa waume zao na watumishi kuwauwa mabwana wanaowafanyia kazi.
Natabiri Mwaka huu ni mwaka ambao utatawaliwa na vifo vitakavyoshtua watu wengi.
Natabiri: Huu ni mwaka wa vijana kushika nafasi za uongozi na kuchukua madaraka na wazee wengi watapoteza nafasi zako hasa katika chaguzi mbali mbali zitazofanyika.
Natabiri malumbano makubwa, vurugu na magomvi kwenye mabunge, wabunge watagombana bila kujali itikadi za vyama vyao.
Natabiri mivutano iliyopo hivi sasa katika vyama haitaharibu vyama husika hasa katika vyama vya CUF,NCCR na CCM.
Natabiri: Kutokea vifo vya ghafla kwa viongozi wa kisiasa waliopo madarakani au Serikalini.
Nashauri:- Serikali iwe makini katika utekelezaji wa shughuli zake kwa sababu kunaweza kuzuka mgogoro mkubwa utakaotikisa nchi.
Natabiri, Rais Jakaya Kikwete kupata umaarufu mkubwa wa kisiasa mwaka huu na atashirikisha wapinzani katika shughuli kadhaa za kiserikali hivyo nyota yake kuzidi kung'aa kitaifa.
Natabiribaadhi ya viongozi wa dini kukumbwa na kashfa mbaya na za kutisha zitakazovunja hadhi zao.

Maalim Hassan Yahya Hussein
 
Mchawi tu huyo hata mimi naweza kutabiri kuwa mwaka huu kuna viongozi watakufa au atakufa,mana wapo wengi viongozi Tanzania kwa hyo kifo kutokea ni kawaida tu mana wapo wengi.
 
hahah hata mie niliona huko issa michuzi nikaguna tu,i dont believe in supernatural things,but i know,kujiona una super powers ni moja wapo ya magonjwa ya akili...hana tofauti na babu wa loliondo lol
 
Mhh mbona inaonekana kabisa ni vitu vya kutunga japokuwa sikatai utabiri kweli upo ila kwa hapa naona imekaa ki siasa zaidi na wala sio ki mafundisho,ili wanasiasa ndo waogope au..? Ila ni mawazo yangu tu,nisingependa na wengine wakubali maoni yangu,kila mtu na imani yake,ila namshukuru sana Maalim Hassan Yahya Hussein kwa kuendeleza yale ambayo yameachwa na kipenzi chetu.. Apumzike kwa amani. Sina mengi ya kuchangia zaidi ya hayo..
 
Sasa kama mtu unatabiri kila kitu huoni kama lazima vitakuwepo vichache kati ya hivyo??
Natabiri mvua kunyesha, pia natabiri mvua kutonyesha!!!
 
utabiri ni mambo ya kimajini majini tu.
sio sawa na unabii wa ki Mungu.
ndio maaana yanatabiriwa mengi ni ya mabaya.
SIAMINI JUU YA UTABIRI WAO.
 
Natabiri, jumapili ya katikati ya mwezi wa 6 JF itakufa kwa wiki moja kisha itafufuka tena.
 
kwa nini anatbiri mambo ya kutisha tisha tuu? Mboa katika michezo na usanii , hajatabiria kitu? Yanga inacheza na zamarek, mechi ambayo kila mwana yanga anataka ushindi. Basi mwalimu, victor Yohana Simba kwa kiarabu maanake ni (hussein Yahaya hassan) tutabirie ushindi wa Yanga?
 
sheikh wetu huyo..tushmfunda kama babake... Sema tunaangalia upepo ukoje,vinginevyo tunamuandlia safu tunayoitaka kwenye chama mwaka huu,kisha tunamwambia aseme atakayegombea nafasi awe na nyota fulani,la sivyo atakufa.... Halafu sisi kiulainiii...
 
Jamani haya anayosema huyu Bw. mbona yapo? Mf. njaa, kufa kwa watu wakiwemo viongozi, mapinduzi ya viongozi kv huko kz mwa Afrika; huyu ana lake jambo katika hiki alichokiita utabiri.
 
Yaani huyu kachelewa sana,hivi kuna watu wanaoamini upupu huu?eti mtabiri katumia vigezo gani?maana vyote alivyotabiri vipo kwa mtu ambae anajua na anafatilia dunia inavyokwenda anajua yote hayo kuwa yapo na yatakuja,sioni utabiri hapo ila naona ujanja tu,
 
baba yake alikuwa anatumiwa na serikali kumtabiria mtu kifo kisha serikali inatekeleza kimya kimya hivyo basi nawashauri baadhi ya viongozi hasa wanaojifanya mstari wa mbele kupambana na ufisadi wakae mkao wa kifo.
 
alaaniwe mtu yule amtegemeae mwanadamu nakumfanya kinga yake,abarikiwe mtu yule amtegemeae mungu..!
 
Eti anatabili kutokea njaa kali kwa sababu jua linawaka sana,Jama huu nao ni utabili?
 
Back
Top Bottom