Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mwanamuziki wa nyimbo za miondoko ya asili, Mrisho Mpoto ameonyesha kusikitishwa kwake na baadhi ya watu kumtukana baada ya yeye kuonyesha kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli
Mpoto amesema kuwa sababu kubwa iliyopelekea yeye kutukanwa ni maneno ya uongo yaliyozushwa mitaani kuwa amesema 'Rais Magufuli ni Mungu'.
Kufuatia madai hayo, Mrisho Mpoto ameandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Instagram.
"Nimepokea matusi mengi, kebehi, na maneno machafu juu ya mimi kuunga mkono utendaji wa Rais Magufuli, kitu ambacho nakiamini kuna kukubaliana kwa kutokubaliana lakini siyo kumtukana mtu mwingine siyo busara hata kidogo, kwa kuwa tu hakusema au hakufanya ambacho nafsi yako ilipenda kusikia".
"Kilichonifanya niandike ujumbe huu ni kuwa nisiwekewe maneno mdomoni ya kuwa nimesema Rais Magufuli ni Mungu, kwa wale ambao hawakuangalia sherehe za MEI MOSI, naomba niseme kuwa hayo maneno siyo ya kweli na yamebadilishwa kutoka kwenye ukweli wa niliosema
"Mimi ni mtu mwenye hofu na Mungu siwezi kusema hivyo, kumekuwa na utamaduni ikitokea mtu anaunga mkono utendaji wa Rais kunaibuka kundi la wapinga Maendeleo na kuanza kutukana. Naomba ijulikane kuwa sababu za kumunga mkono Rais, yale niliyokuwa nayaongea huko nyuma naona yanafanyiwa kazi hivi sasa"
"Mrisho Mpoto mpaka sasa namuunga mkono Rais Magufuli, iwe nachumia tumbo kwa inavyosemwa au nimevimbilwa kwa shibe". alisema Mpoto