Mrembo ndotoni

Mrembo ndotoni

Rauyah

Member
Joined
Jan 21, 2014
Posts
28
Reaction score
13
Wanajamii nawasalimu.

Kila mtu huwa na Ndoto na njozi.Kwa Muda wa wiki mbili sasa nimekuwa nikiota ndoto ya ajabu.Ndani ya ndoto hiyo namuona binti mrembo akiwa amesimama kando ya bahari huku gauni lake la samawati likipeperushwa na upepo mwanana wa bahari.Sura yake ni ya mviringo na yakuvutia.Macho yake yanaita vilivyo.Vidani vyake vinawaka mithili ya nyota.Hereni masikioni,mkufu shingoni,bangili mikononi na vikuku miguuni.Mara nyingi namuota akiwa anacheza taratibu na kwa mahaba.Mara nyingine huwa amesimama tu akiangalia baharini huku upepo ukipuliza nywele zake za singa.Kila napojaribu kumgusa ndo huwa nashtuka nakujikuta niko mwenyewe kitandani.Sura yake sijawahi kuiona sehemu nyingine zaidi ya kwenye hiyo ndoto.Kinachonishangaza ni kwamba ndoto hii hujirudia mara kwa mara.

Jamani naomba wenyekujua kutabiri ndoto wanidadavulie maana naanza kupata woga.Au ndo jini mahaba huyu?
 
Huyo ni jini mahaba omba sana kama uko kwenye ndoa hamu yamkeo itapotea nakama uko na mtaanZa gombana hakuta kuwa na maelewano so nenda kwenye maombezi watakusaidia
 
Huyo ni jini mahaba omba sana kama uko kwenye ndoa hamu yamkeo itapotea nakama uko na mtaanZa gombana hakuta kuwa na maelewano so nenda kwenye maombezi watakusaidia

Asante sana kwa ushauri,kwa kifupi sijaoa ila nina demu ambaye bado hatujaingia rasmi kwenye uchumba.Inanitisha sana aisee.
 
Kama anaimba taarbu huyu atakuwa ni isha mashauzi. Ndiye mwenye vidana wili mzima. Otherwise hiyo ni ndoto tu haina uhusiano wowote ule na hali halisi. Ndoto hutokana na mawazo unayowaza kabla ya kulala
 
jiandae kuoa jini,ndg kuna dada alinipa story,toka mwaka 2005 alikuwa anaota anafanya mapenzi na mtu asiye mjua,mwisho we,akfunga ndoa naye kanisani akiwa ndoton.kilichotokea,hana hamu ya mapenz na muwewe,na kila akishika mimba zinatoka,baada ya kuzunguka kwa wataalam ikabainika ,aliolewa na jini bila kujua,sa ndo anapata tiba
 
Unazidi kunitisha...Itabidi nizame kwenye maombi mazito.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom