Mrema: Mimi si kibaraka wa CCM

Mrema: Mimi si kibaraka wa CCM

Mrema ni mganga njaa tu hana lolote. Amejichokea zake hana jipya, haoni haya wala vibaya.
 
ha ha ha kuna siku tulikuwa tuko kwenye kampeni zake za uraisi niliambana naye tukiwa njiani sanduku lake likadondoka kutoka mahali lilipo kuwa vitu vyake vikamwagika tulicho shuhudia ni wingi wa condom alizokuwa nazo kwenye bag yake watu walicheka sana.
Huyu mrema ni majanga na alikuwa anasema anajua awezi shinda uraisi na hata ikitokea ameshinda anajua awezi pewa uraisi


Duu Mkuuuu wewee ni kiboko hii imenivunja mbavu zanguuu, kwani hizo condom alikuwa anaenda kuzitumia kwenye mkutano wa kampeni? Sasa ninajua kwanini huyo jamaa anakuwa anaumwaumwa lazima atakuwa amekanyaga gridi ya taifaaaa
 
Mrema hajawahi hata kuanzisha chama. Alikaribishwa NCCR akakiharibu. Akakaribishwa TLP na amekifanya kama mali yake. Aliingia tu upinzani mara tu baada ya kutoswa na CCM baada ya kutofautiana nao kwa vile hakutaka kuficha uchafu wa CCM kama ilivyo desturi ya chama. Ukitaka udumu CCM ni lazima Ujue kula na kipofu. Vinginevyo wanakupoteza.
 
Mrema kula mafao yako sidhani kama 2015 utarudi
 
Kama sio kibaraka basi ana bwa.na pale sisiemu
 
hata mlevi hasa wa mataputapu huwa hajitambui kuwa kalewa,
 
Leo hii baada ya kiongozi wa upinzani bungeni mh Mbowe kutolewa nje, akichangia bungeni amesema yeye si kibaraka wa CCM kama watu wanavyodhani na kuwasema sana CHADEMA kwa vitendo vyao vya kutoka nje.

Mrema anaogopa akitoka nje watamnyima ile pension ya cheo feki cha naibu waziri mkuu. Ghasia alishamwambia cheo hakipo kikatiba bado akaenda kuomba kwa Kikwete. Naye JK kama kawaida akasema alipwe akijua ni kinyume cha sheria. Labda alipwe kisiri. Akilipwa tu tunaenda mahakamani tuje amelipwa kwa sheria na kanuni ipi.
 
Huyu siye Agustino Lyatonga Mrema niliyekuwa namfahamu! Sio yule aliyekwenda uwanja wa ndege kukamata dhahabu zilizokuwa zinasafirishwa kwenda nje na vigogo fulani! Sio yule aliyekuwa mstari wa mbele kufichua ufisadi na maovu yote! Huenda ni uzee na kama ni huyo kweli kazeeka vibaya. Anabomoa yale aliyoyajenga! Poleni TLP na watu wa Vunjo!
 
Jamani kuweni na huruma, hiki kidingi kinatafuta mazishi ya kiserikali.
 
Babu ambirikile muongezee doz ya kikombe mpe 2 maana naona ugonjwa wake umekula ubongo uwezo wa kufikir umepungua.
 
Back
Top Bottom