Mrema: Mimi si kibaraka wa CCM

Mrema: Mimi si kibaraka wa CCM

DJ NYUKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2013
Posts
370
Reaction score
89
Leo hii baada ya kiongozi wa upinzani bungeni mh Mbowe kutolewa nje, akichangia bungeni amesema yeye si kibaraka wa CCM kama watu wanavyodhani na kuwasema sana CHADEMA kwa vitendo vyao vya kutoka nje.
Mzee wa kiraracha alimuomba Pinda msamaha kwa kujaza fomu yakutokuwa na imani naye adai aliburuzwa tu.
 
Ni kweli si kibaraka, na wala si mpinzani. Yupo ama hayupo yote sawa. Sina hakika kama ni yuleyule Mrema wa NCCR ama alibadilishwa. Kwa sasa hakuna tofauti kati ya Mrema na mwigulu, na afadhali Mwigulu ni mjuzi wa ujasusi.
 
mrema hajawahi kuwa mpinzani,ukijumlisha na ugonjwa wake ndio anazidi kujipendekeza ccm kwa ajili ya matibabu.
 
Yeye anasubiri kupewa mafao ambayo hayapo katika taratibu za utumishi wa umma kwa kuhongwa na maccm!
 
Alishapewa kiinua mgongo chake huyu ndio maana hawezi kuisoma CCM kwani bado haja pesa zote ....amejenga Guest house Dodoma eneo la area D inaitwa Kiraracha.
 
Mrema ni mpinzani wa upinzani! jamaa ni radical sana sema njaa huwezi pigana nayo! Adui wako mwombee njaa! Sasa Mrema kapigana weeee, akaja jikuta kama amezungukwa na makachero kila upande! Akaona cha kufia nini??? Kama huwezi pigana nao basi ungana nao????
 
Mzee wa Kiraracha Maradhi yamehamia kwenye ubongo. Msameheni bure, yuko kwenye hali ngumu kimaisha!
 
Bora anyamaze kimya asidhani kuna watu wajinga. Mrema aliomba apewe jimbo la Vunjo na akapewa baada ya kucheza kiduku kwenye mkutano wa CCM kule Dodoma. Huyu hajawahi kuwa mpinzani. Ni mnafiki aliyekubuhu. We have to know that old age is not an investment. Ukitaka kuthibitisha hili kumbuka mchango wa Kingunge kwenye Rasimu ya Katiba kuhusiana na serikali tatu. Brain imekuwa senile.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ningukuwa na number yake ningemwambia asisumbuke kutuambia haya maana sisi hatujaondolewa akili za kutambua nani ni nani ndani ya bunge na hata nje.
Yeye abembeleze tu mafao yake cuz akili yake siku hizi imeishia kwenye hio ruzuku ya kasaccoss kake ka tlp na mafao ya kuhongwa.
 
ha ha ha ha njaa ni kitu mbaya sana...mrema huyuhuyu? jamani mbona alivokua akiongea leo hakuacha shaka yoyote kwamba yeye si kibaraka kama kweli si kibaraka kwa nini hakuchangia moja kwa moja badara yake akaanza utuetezi
 
Ni kweli, tumuache mzee huyu apumzike, ila kwa kuheshimu lile jina la enzi zake la MREMA, napendekeza sasa abadilishe jina na kuitwa LYATONGA WA KIRARACHA, ili kulinda heshima ya yule mwanamageuzi machachari wa wakati ule
 
ha ha ha kuna siku tulikuwa tuko kwenye kampeni zake za uraisi niliambana naye tukiwa njiani sanduku lake likadondoka kutoka mahali lilipo kuwa vitu vyake vikamwagika tulicho shuhudia ni wingi wa condom alizokuwa nazo kwenye bag yake watu walicheka sana.
Huyu mrema ni majanga na alikuwa anasema anajua awezi shinda uraisi na hata ikitokea ameshinda anajua awezi pewa uraisi
 
Babu Mrema is a spent force sijui mawazo yake siku hizi yanalenga wapi. Mkiti wa TLP lakini urais 2015 kampeni kwa Lowasa kisa ni fisadi! Babu pumzika hata huko bungeni wana Vunjo hawaambulii chochote bora CDM ingechukua Vunjo ungekuta mambo shwari kwani wangepata mtetezi mzuri wa katiba mpya.
 
"Kwani bungeni tunaenda kubeba tofali?
"hilo ndo bonge la point alitema pale Moshi Fm.
 
ha ha ha kuna siku tulikuwa tuko kwenye kampeni zake za uraisi niliambana naye tukiwa njiani sanduku lake likadondoka kutoka mahali lilipo kuwa vitu vyake vikamwagika tulicho shuhudia ni wingi wa condom alizokuwa nazo kwenye bag yake watu walicheka sana.
Huyu mrema ni majanga na alikuwa anasema anajua awezi shinda uraisi na hata ikitokea ameshinda anajua awezi pewa uraisi

kwa hiyo huo mfano unahusiana na hali yake ya sasa hivi? nifikiriavyo mimi ni kuwa kakamatwa ufahamu kitambo wala hajitambui
 
leo hii baada ya kiongozi wa upinzani bungeni mh mbowe kutolewa nje.akichangia bungeni amesema yeye si kibalaka wa ccm kama watu wanavyo thani.na kuwasema sana chadema kwa vitendo vyao vya kutoka nje.

mrema ni kibaraka bana.ukimpekua utamkuta na kadi ya ccm.!!!!!nccr kiliundwa kwa madhumuni ya kuwadaka viongozi ambao wangeikimbia ccm wakati vyama vingi vilivyoanzishwa!!!lengo ni kuunda chama kidogo cha kiufundi.wakaja kukiulia tanga.mkuu wa mkoa wa tanga enzi hizo alikuwa hassy kitine kama sikosei.hassy kitine hakuwa uwt?????
 
Mzee wa kiraracha alimuomba Pinda msamaha kwa kujaza fomu yakutokuwa na imani naye adai aliburuzwa tu.
 
Inaelekea wabunge wa ccm ndio wateja wakubwa wa bar yake inayoitwa kiraracha hapo dodoma.
 
Back
Top Bottom