Mrema afungua kesi Mahakama kuu Moshi kupinga ushindi wa James Mbatia

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
attachment.php


Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Vunjo Augustino Mrema amefungua kesi Mahakama Kuu Moshi, kupinga matokeo ya Uchaguzi yaliyomtangaza James Mbatia wa NCCR-Mageuzi mshindi.

Mbatia alishinda Ubunge katika jimbo hilo kwa jumla ya kura 60,187 aliyemfuata ni Innocent Shirima aliyepata kura 16,617 na Mrema alipata kura 6,416.

Mrema amemtuhumu Mbatia, Mkurugenzi wa Uchaguzi Vunjo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kukiuka baadhi ya taratibu za uchaguzi.

Akiongea na waandishi baada ya kufungua kesi amesema, "amesema nimeamua kufungua kesi kwa sababu nataka haki yangu"

Ameiomba Mahakama kufuta matokeo ya Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo hilo na kutaka uchaguzi urudiwe.

Kwa mujibu wa Ndugu Mrema, James Mbatia alisambaza karatasi za kupigia kura kabla ya siku ya uchaguzi akitaka wananchi wampigie kura, amesema kuwa Mbatia alisambaza karatasi za kupigia kura mpaka makanisani na kwenye misikiti.
 

Attachments

  • mbatia_clip.jpg
    mbatia_clip.jpg
    19.7 KB · Views: 6,293
"Mrema amemtuhumu Mbatia.. Mkurugenzi wa Uchaguzi Vunjo.. na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.." Huyu mzee sasa bora bwana JPM ampe tu ukatibu kata.. maana hata kwa hiyo tofauti ya kura bado anataka uchaguzi urudiwe. Au wapiga kura watakuwa wengine!??
 
Ukirudiwa wapiga kura watakuwa walewale!!??? Maana kura 60,000 kwa 6,000!
 
"Mrema amemtuhumu Mbatia.. Mkurugenzi wa Uchaguzi Vunjo.. na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.." Huyu mzee sasa bora bwana JPM ampe tu ukatibu kata.. maana hata kwa hiyo tofauti ya kura bado anataka uchaguzi urudiwe. Au wapiga kura watakuwa wengine!??

Mahamakama itaamua, tusimbeze.
 
Namuunga mkono, ila aongeze washitakiwa kuwa hata hao wapiga kura, kwa nini wamchukie kiasi hicho. Si wangempa kura nyingi kidogo hata afikie 30.000 ziwe nusu ya Mbatia? Hawajui kuwa alikuwaga mbunge wao?? Aliwatenda nini mpaka wachukie kiasi hicho wamfanye wa 3??
Go, go, mh. Mrema, Naibu pekee wa Waziri Mkuu katika historia ya Tz.
 
Mzee wa Kiraracha anatokwa na mipovu,hata aibu haoni yani tofauti ya kura almost 54,000 elfu
 
Huyu mzee akili zake anazijua mwenyewe. Kabla ya mageuzi hayajashika hatam Tanzania, mwaka 2006 alipigiwa kura kwa wingi kule Temeke. Akawa mmoja ya wabunge wachache wa upinzani. Hee, mara tu akaanzisha mtafaruku ndani ya NCCR-Mageuzi akaacha na ubunge wenyewe. Wananchi wa Temeke hawajamsamehe mpaka leo.
 
Back
Top Bottom