Mrema aandaa mkutano wa kujitangaza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrema aandaa mkutano wa kujitangaza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lucchese DeCavalcante, Nov 3, 2010.

 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Daniel Mjema,Moshi

  MBUNGE Mteule Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP),Agustino Mrema,
  Jumamosi wiki hii atafanya mkutano mkubwa wa hadhara kutangaza mambo atakayowafanyia wananchi
  wake ndani ya siku 100.

  Mkutano huo utakakaofanyika katika mji mdogo wa Himo kuanzia saa 4:00 asubuhi,
  utatanguliwa na maandamano makubwa yatakayohusisha magari, waendesha pikipiki
  na wananchi kutoka kata zote za Jimbo hilo.

  Akizungumza na Mwananchi jana, Mrema alisema angefurahi sana kama waliokuwa wapinzani
  wake katika kinyang’anyo cha Ubunge nao watahudhuria mkutano huo kwa kuwa nao ni wakazi wa Jimbo hilo.

  “Ningefurahi sana kumuona rafiki yangu na mtoto wangu Chrispin Meela na
  John Mrema waje tu wasione soo (aibu) kuja kumsikiliza Mbunge wao atawafanyia nini
  ndani ya siku 100 madarakani kwa sababu siasa si uhasama”alisema.

  Katika kinyang’anyiro hicho,Mrema ambaye pia ni mwenyekiti wa
  Taifa wa TLP alipata kura 38,010 akifuatiwa na mgombea wa
  Chrispin Meela kura 23,870 huku John Mrema wa Chadema akipata kura 6,316.

  Mrema alisema alisema matumaini ya Wananchi wa Jimbo hilo kwake ni makubwa sana
  hivyo anataka atumie mkutano wa Jumamosi kuwashukuru kwa kumchagua na pia
  nini atawafanyia ndani ya siku 100.

  SOURCE: Gazeti la Mwananchi
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  jamaa bado hajaacha mikwala yake :smile:
   
 3. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Good!
   
 4. E

  Edo JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  safii; he knows the game very well, shukrani na action plan ni muhimu
   
Loading...