Mrejesho wa mpenzi wangu 'mtoto'

Mrejesho wa mpenzi wangu 'mtoto'

Meridah Tough

Senior Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
136
Reaction score
365
Wako habari zenu.

Mara kadhaa nimekuwa nikileta mada juu ya mahusiano yangu na kwa kweli nashukuru sana wanajukwaa kwa ushauri mbalimbali ambao kiukweli nimefaidika sana.

Baada ya mivutano mingi baina yangu na mwanaume huyo ambaye niliwahi kulalamika hapa kuwa hajui nini anahitaji katika maisha yake, sababu anakuwa na wanawake wengine hata kuonana nao hajawahi kuonana nao.

Kwa kweli, hali hiyo ilininyima raha na nikiona sababu ya kuendelea kuwa katika mahusiano hayo. Nikaamua kujiweka pembeni. Haikupita wiki, huyu jamaa alinitafuta na kuniomba tufungue ukurasa mpya na hizo tabia za wanawake hataziacha.

Kiukweli, trust juu yake nimeshtuka sana. Na niliona wazi hata nikirudi kwake, hatutadumu. Hivyo, nilimpa masharti ya kuthibitisha kauli yake kwa vitendo. Tujicommit na hata tufunge ndoa.

Hapo jamaa hakujibu chochote, na siku ya pili yake, alinitafuta kana kwamba hakuna nilichomwambia. Hapo ilinibidi kuwa mkali na nikamwambia kama hawezi kucommit, aendelee na mambo yake na asinitafute.

Kwa wale ambao mnadhani nimemzimikia sana jamaa, mpo sahihi. Lakini kamwe siwezi ruhusu hisia zangu zikanifanya niishi maisha yasiyo na future. And am so ready kufanya maisha mengine.
 
Kwahiyo tatizo kwako siyo tabia yake ya kukusaliti na kupenda hata wanawake wengine hasiowajua? Ila tatizo lako wewe kwa sasa ni ndoa!

Hakika nakuambia, tabia ni Kama ngozi ya mwili hata akuoe huyo mwanaume kamwe hatabadilika. Kama shida ni ndoa mm nilishatafuta ukumbi na padre wakufungisha ndoa pia yupo nishamtafuta. hapa nimebakiza kutafuta mwanamke tu wa kuoa. Kama uko tayar njoo inbox🤔
 
Subiri nikuquote kabisa ili usije kunigeuka. "Huyu jamaa alinitafuta na kuniomba tufungue ukurasa mpya na hizo tabia za wanawake hataziacha". Unalalamika nini sasa.
Labda nimekosea maana "hataziacha" ninamaanisha hatozifanya tena. Anaachana nazo.
 
Sitaki nataka..inshort hamna sehem unaenda subiri upigwe kombola moja kwanza la heart break ndo utafanya maamuzi seriouse

SUBIRI KIDOGO
Mkuu umewahi kukaa kwenye mahusiano ambayo umechoka kuona drama kila siku? Ndio situation ambayo ninayo. Nimechoka. Nimegive up. Ningekuwa nataka kurudi aliponitafuta tu, ningemkimbilia. Na siwezi kurudi unless nione vitendo vimebadilika. Ndipo trust yangu inaweza kuanza kujijenga upya. Sasa hivi nikirudi, sitakuwa na amani wala furaha. Simuamini.
 
Kwahiyo tatizo kwako siyo tabia yake ya kukusaliti na kupenda hata wanawake wengine hasiowajua? Ila tatizo lako wewe kwa sasa ni ndoa!

Hakika nakuambia, tabia ni Kama ngozi ya mwili hata akuoe huyo mwanaume kamwe hatabadilika. Kama shida ni ndoa mm nilishatafuta ukumbi na padre wakufungisha ndoa pia yupo nishamtafuta. hapa nimebakiza kutafuta mwanamke tu wa kuoa. Kama uko tayar njoo inbox🤔
Hapana. Tena mimi ni muoga wa ndoa. Ila akijicommit, hawezi kufanya mambo ya namna hiyo. Trust me. But kwa sasa hata nimkute na mwanamke mwingine, mimi nalalamika kama nani? Yan mi ni nani yake? So kama yupo serious tujicommit.
 
Ulipata mtoto
 
ndoa haijawahi kuwa commitment ya uaminifu, ukipenda boga penda na ua lake. Kweli mapenzi upofu nimeamini. Anyway kila kheri dada.
 
We unachotaka ni ndoa!!! Tafuta mwanaume achana na huyo mvulana

Ila wadada poleni maana sometimes ili ufikie ndoa lazima upitie changamoto nyingi sana.
 
Ulipata mtoto
Niliogopa, maana mtu mwenyewe kwa kweli. Ananipa kigugumizi
 
Mkuu ningekuwa na trust kwake, nisingemwambia ajicommit.
Ninaogopa kurudi tena, tukaendeleza yaleyale. Kuna vitu vingi tumepitia. Ingawa sijaviandika vyote. Ule uaminifu haupo tena. Hata mtu akikuandikia msg kuwa anakupenda, huoni wala kusikia chochote. Ni kama umeona msg ya mtu wa kawaida tu.
Kwa hiyo sina trust iliyobaki juu yake. Kila anachokiongea naona ni uongo. So ili kurudisha uaminifu lazima afanye vitendo fulani vya kunifanya mimi nianze kujenga trust juu yake. Maneno tu nimeyachoka. Maana huko nyuma alisema ila alifanya tofauti. Now tuhamie kwenye vitendo.
Hata kama kuna kitendo chochote mbali na ndoa, nipo tayari.
 
Wako habari zenu.

Mara kadhaa nimekuwa nikileta mada juu ya mahusiano yangu na kwa kweli nashukuru sana wanajukwaa kwa ushauri mbalimbali ambao kiukweli nimefaidika sana.

Baada ya mivutano mingi baina yangu na mwanaume huyo ambaye niliwahi kulalamika hapa kuwa hajui nini anahitaji katika maisha yake, sababu anakuwa na wanawake wengine hata kuonana nao hajawahi kuonana nao.

Kwa kweli, hali hiyo ilininyima raha na nikiona sababu ya kuendelea kuwa katika mahusiano hayo. Nikaamua kujiweka pembeni. Haikupita wiki, huyu jamaa alinitafuta na kuniomba tufungue ukurasa mpya na hizo tabia za wanawake hataziacha.

Kiukweli, trust juu yake nimeshtuka sana. Na niliona wazi hata nikirudi kwake, hatutadumu. Hivyo, nilimpa masharti ya kuthibitisha kauli yake kwa vitendo. Tujicommit na hata tufunge ndoa.

Hapo jamaa hakujibu chochote, na siku ya pili yake, alinitafuta kana kwamba hakuna nilichomwambia. Hapo ilinibidi kuwa mkali na nikamwambia kama hawezi kucommit, aendelee na mambo yake na asinitafute.

Kwa wale ambao mnadhani nimemzimikia sana jamaa, mpo sahihi. Lakini kamwe siwezi ruhusu hisia zangu zikanifanya niishi maisha yasiyo na future. And am so ready kufanya maisha mengine.
naomba nitafute pm kama hutojali
 
Hongera kwa akili zako kuweza kushinda moyo Meridah Tough hiki ni kitu kinachowashinda wengi
Kosea kwengine kote ila sio kwenye ndoa
 
Ndoa sio kigezo tosha cha uaminifu.
Je? Umejaribu kufikiria maisha baada ya ndoa kama akikubari kufunga ndoa na wewe?

Ukiona hauop sehemu sahh usikimbilie kujicommit kwenye ndoa kwa kuisi ndio kifungo cha uzinzi/umalaya kwa mwenza wako, Mwambie SIKUTAKI HATUENDANI bas na ww ondoka usigeuke nyuma.
 
Back
Top Bottom