sweetapple
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 533
- 461
Natumaini mu wazima wanajamvi wote,
Napenda kuchukua nafasi hii kuelezea ya moyoni na hali ilivyokuwa baada ya post yangu yenye kichwa hapo juu, japo uzi ule uliombwa ufutwe baada ya kuleta madhara.
kabla ya yote, naomba nirudie kukiri hadharani kwamba nampenda mchumba wangu, pamoja na yote yaliyotokea but still nampenda tena sana na kuwaza eti tunatengana au tumetengana ni jambo linalofikilisha sana pamoja na kunikondesha.
Sawa kama binadamu anaweza akawa aliteleza na mimi kuchukua uamuzi wa
haraka kuja kulalamika jambo lililozua rafrani kubwa ambayo mwanzo sikutegemea, mwanzo nilijua naamini rningepata tu ushauri, lakini ushauri ukanichukua na mimi kuanza kumponda. Naomba msamaha kwa niaba ya watu walioteleza kushauri kupitiliza pamoja na yote kama nilivyowai sema toka mwanzo hapo mengi mazuri aliyonifanyia, nitakuwa mchoyo wa fadhira nikiangalia upande mmoja tu wa shilingi. Nia yangu ya mwanzo ilikuwa kuona ushauri wa wengine kama ipo sawa.
Lakini badala ya kujenga ikabomoa. Mapenzi yanaumiza sana hasa kwa mtu unayempenda sana, kuandika inaweza ikawa rahisi sana lakini katika uhalisia ikawa ngumu sana. Kama nilivyokuja mwenyewe hadharani na kuwashirikisha mkasa wangu na ushauri wenu wote nashukuru lakini ndani ya nafasi yangu naumia sana. Nashindwa kuwa normal kwa kumkosa.
Japo nashukuru Mungu tumeanza kuwasiliana baada ya wiki mbili naamini Mungu atatupigania tena na kujirekebisha pale wote tulipoteleza. Kazi ya shetani ni kuona watu wake wakikosa amani na kuwatenganisha kwa namna yoyote ile. Naomba wanaJF wenzangu haaa wale wanaomwamini Mungu mtuombee mimi na mchumba wangu wa maisha tuzidi kuamini katika Mungu na kumkemea shetani aliyejaribu kututenganisha kwa hila.
Mpenzi naomba nisamehe sana, nia yangu haikuwa kukuaibisha au kukufanya ujisikie vibaya bali nilikuwa najaribu njia mbadala ili uone ni wapi naumia. Kwa yote yaliyotokea najua ni mitihani sisi sio wa kwanza kupitia jaribu hilo wapo wengi na kikubwa ni kuombeana na kufanikisha yale tuliyokwisha anza na kufika mbali.
Ahsante.