Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,185
- 7,491
Wakuu nawasalimu.
Nilitangaza nafasi ya kazi humu ya usimamizi wa biashara ambapo kigezo cha kwanza nilichokuwa nimetoa ni uaminifu.
Nafasi ya kazi kwa mtu mwaminifu sana
Matokeo ni kama ifuatavyo:
(a) Watu 81 waliomba kazi hii.
(b) Watu 29 walijibu maswali niliyouliza ya kupima uaminifu na wakathibitisha kuwa uaminifu wao hauna shaka, hivyo kupita kwenye hatua ya kwanza ya usaili.
(c) Katika hatua ya pili ya usaili, nilichagua waombaji 15 kutoka kwenye 29, hapo juu, nikawatumia fedha kwa tigo/mpesa kwenye namba walizonipa (kutoka kwenye namba wasiyoijua bila maelekezo yoyote.
Kiwango nilichotuma kwa kila mmoja ni kati ya ya 2000 - 10,000/=. Kati ya hao 15, 13 walipokea hela wakazilamba bila hata kuuliza mtumaji kama alikosea namba au alituma kwa makusudi na kama alituma kwa makusudi alituma za nini.(hatua hii imewafanya kushindwa usaili).
Watu wawili waliuliza, nikawambia nimetuma kwa makosa, wakaonesha dhamira ya kunirudishia ndio nikawajulisha kuwa ilikuwa ni sehemu ya pili ya usaili wa kazi hii. (hao wawili wamefaulu usaili kwenye hatua hii) na kati yao mmoja atapewa kazi.
Nawatakia kila la heri.