Mrejesho:Mama Niliyempa Lifti

Mrejesho:Mama Niliyempa Lifti

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,270
Halo Wanammu
Natinga tena hapa ukumbini kuendeleza kisa kilichonikuta nilipompa mama mmoja lifti kama nilivyosimulia kwenye thread hii:Wewe mwanamke, wanifahamu sana mimi pamoja na mke wangu: Kwanini ufanye hivyo?.

Nilijawa na usongo mwingi sana wa kumpata huyo mama ili anieleze sababu za kumweleza mke wangu kwamba nilimpa huyo mama lifti.
Kama kawaida yangu kila Jumamosi naenda Bomang'ombe kutembea na jumamosi ya tarehe 9 mwezi huu mara paap nakutana naye akitoka sokoni."Haa Shieka", alianza, "hujaenda dodoma wewe kwenye sherehe?"

"Sijapata lifti ya kwenda huko" nilimjibu kwa makusudi kumkumbushia.Na kweli akakumbuka akaniuliza kama nilifanikiwa kupata shamba la mpunga.Sikumjibu ila nilimwuliza kwa nini alimweleza mke wangu juu ya lifti niliyompa.

"Nani? Mimi?", aling'aka.
Alikataa katakata kwamba yeye hawezi kufanya kosa hilo la hatari ila pengine rafiki yake aliyemtembelea baada ya kushuka kwenye lift."Sikia Shieka," aliniambia, "Nilipitia kwa rafiki yangu akaniuliza nimewahije kufika Rundugai, miye nikamwambia baba mmoja kwa jina la Shieka alinipa lifti"
Nilimwuliza kama huyo rafiki yake ananifahamu mama akasema ananifahamu sana mpaka nyumbani kwangu.

Hapo nikapata picha, nikaelewa jinsi mke wangu alivyopata habari.
Kama ni lawama, simlaumu niliyempa lifti ila lawama nazielekeza kwa yule aliyeambiwa halafu yeye kaona kuna habari muhimu ya kumkimbizia mke wangu.

Ni mambo ya akina mama hayo, ila kuna baadhi ya wanaume wana tabia hizo za kutembeza 'habari'

Jamaniee, Nawatakieni Krismas yenye amani na furaha isiyokuwa na vyuma vilivyokaza
 
huu mrejesho hata usingeuleta humu, ungebaki nao tu
 
Dyuuuuu kwa hiyo umeamua kuja kupumzika kwa hiyo thread
 
😀😀😀😀😀
Muwage mnatoa mbegu kabla ya kuvuta...
Hukumla nyama?😀
Halo Wanammu
Natinga tena hapa ukumbini kuendeleza kisa kilichonikuta nilipompa mama mmoja lifti kama nilivyosimulia kwenye thread hii:Wewe mwanamke, wanifahamu sana mimi pamoja na mke wangu: Kwanini ufanye hivyo?.
Nilijawa na usongo mwingi sana wa kumpata huyo mama ili anieleze sababu za kumweleza mke wangu kwamba nilimpa huyo mama lifti.
Kama kawaida yangu kila Jumamosi naenda Bomang'ombe kutembea na jumamosi ya tarehe 9 mwezi huu mara paap nakutana naye akitoka sokoni."Haa Shieka", alianza, "hujaenda dodoma wewe kwenye sherehe?"
"Sijapata lifti ya kwenda huko" nilimjibu kwa makusudi kumkumbushia.Na kweli akakumbuka akaniuliza kama nilifanikiwa kupata shamba la mpunga.Sikumjibu ila nilimwuliza kwa nini alimweleza mke wangu juu ya lifti niliyompa.
"Nani? Mimi?", aling'aka.
Alikataa katakata kwamba yeye hawezi kufanya kosa hilo la hatari ila pengine rafiki yake aliyemtembelea baada ya kushuka kwenye lift."Sikia Shieka," aliniambia, "Nilipitia kwa rafiki yangu akaniuliza nimewahije kufika Rundugai,miye nikamwambia baba mmoja kwa jina la Shieka alinipa lifti"
Nilimwuliza kama huyo rafiki yake ananifahamu mama akasema ananifahamu sana mpaka nyumbani kwangu.
Hapo nikapata picha, nikaelewa jinsi mke wangu alivyopata habari.
Kama ni lawama, simlaumu niliyempa lifti ila lawama nazielekeza kwa yule aliyeambiwa halafu yeye kaona kuna habari muhimu ya kumkimbizia mke wangu.

Ni mambo ya akina mama hayo, ila kuna baadhi ya wanaume wana tabia hizo za kutembeza 'habari'

Jamaniee, Nawatakieni Krismas yenye amani na furaha isiyokuwa na vyuma vilivyokaza
 
huu mrejesho hata usingeuleta humu, ungebaki nao tu
Ebo! Mkuu, ulishaona ukiletewa chakula mezani ukala ukashiba meza ikaachwa hivyohivyo bila kusafishwa?
 
Back
Top Bottom